80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

HOJA ZA M600 NA M80 NI HOJA DHAIFU SANA........


-Klabu ya Yanga Sc leo itacheza mchezo wa marudiano wa mtoano wa Caf Confederation Cup na timu ya Welayta Dicha ya Ethiopia mchezo wa mkondo wa kwanza klabu ya Yanga ilishinda kwa magoli 2-0

-Yanga inahitaji kutofungwa zaidi ya goli moja na Dicha ili iweze kufuzu hatua ya makundi ya Caf Confederation Cup iwapo Klabu ya Yanga Itafuzu Makundi ya Kombe hili itapata kitita cha milioni 600 za kitanzania kama zawadi ya kufanikiwa kutinga makundi.

-Sasa kumeibuka dhana ya Hoja ya kwamba eti bora milioni 600 kuliko milioni 80 unajua wamaanisha nini bora kufuzu makundi ya kombe la shirikisho wapate milioni 600 kuliko kuchukua ubingwa wa Tanzania Bara (vpl) maana Bingwa wa ligi kuu Tanzania Bara anapata milioni 80.

-Ni hoja Dhaifu muno na ni Mbinu za kisungura  ambazo kwa watu wa mpira zinatakiwa kuzikataa kata kata huwezi ukasema bora milioni 600 kuliko milioni 80 wakati ushindi wa milioni 80 ndio uliofanya timu izifikie hizo milioni 600 huwezi kucheza makombe ya Afrika bila kushinda makombe ya Azam Sports Federation Cup na Ligi kuu Tanzania Bara (vpl) ndio utapata nafasi ya kuzitafuta milioni 600 au bilioni 1.2

-Hoja Hii dhaifu imeanza kuingia kwa baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga na kuamini bora milioni 600 kuliko milioni 80 hadi baadhi ya wachezaji wameanza kuingia kwenye mtego huu wa Sungura wakiamini milioni 600 ni bora zaidi kuliko milioni 80

-Badala ya kuamini zote ni bora na hiyo ndogo ni bora zaidi maana ndio njia au daraja linalokufanya ufike huko mbele. Yanga walikuwa mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara na walishiriki kombe la klabu bingwa Africa (Caf Champions League) na ilibaki kidogo tu waingie makundi ya Caf Champions League niwakumbushe tu iwapo Klabu ya Yanga wangeingia makundi ya Champions wangepata bilioni 1.2 fedha ambayo ni kubwa na ingekuwa msaada kwa klabu hiyo.

-Hata hii milioni 600 kwa sasa ni kubwa sana ila isiwe dharau baada ya kuvuka mto unaweza ukakosa kote kote ikawa shida juu ya shida. Naamini Yanga watafuzu Makundi ya Caf Confederation Cup je msimu ujao itakuwaje kama hii milioni 80 walishaikatia tamaa tayari? Maana yake ni kwamba wamekubali Simba wawe mabingwa wa vpl huku Kwenye kombe la Asfc walishatolewa je watapataje milioni 600 msimu ujao? Au ndio hizo zimewatosha watazitumia kwa misimu miwili?

-Tuache stori za Sungura sizitaki mbichi hizo,  Sungura baada ya kushindwa kuzifikia ndizi akaaza kuziponda ndizi zenyewe mbichi hata hazitaki wakati alikuwa nahangaika kuzitafuta ndivyo Yanga wanavyoanza kuingiza hoja dhaifu ya milioni 80 et ndogo na za nini wakati na wao wanashiriki ligi kuu na wako kwenye mbio za ubingwa  au na wao wamekuwa Sungura baada ya kuona hali sio nzuri ndio wanasema sizitaki milioni 80 hizo kwanza ni ndogo kweli jaman kweli? Musikubali hoja dhaifu ziwatawale kwa sasa.

-Pia hii ni faida kwa taifa iwapo Yanga watafanya Vizuri na kufika mbali kwenye kombe hilo tutapanda kwenye rank ya vilabu kwa taifa kwa sasa Tanzania tupo nafasi ya 16 tukiwa na point 5 huku Misri wakiongoza na pointi 85 wakati anayeshika nafasi ya 12 ni Nigeria ana pointi 13 kwa Rank ya mwaka 2017.

-Assume Yanga afike hata nusu fainali ya Caf tutapata pointi ambazo zinaweza kufika 10 then msimu ujao Timu za Tanzania zifanye vizuri na kuwe na mikakati ndani ya shirikisho na vilabu vyenyewe ndani ya misimu 5 tufanye kitu tunaweza kuingia kwenye nafasi ya 12 kwenda juu mataifa ambayo yanatoa timu 4 kwenye michuano ya Caf ikiwa 2 Caf Champions League na 2 Caf Confederatio Cup.

Hizi story za Sunguru waàchieni watu ambao sio wa Mpira.

@yossima Sitta Jr.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE