ZLATAN IBRAHIMOVIC ATIMKA MAN UNITED
Jana jioni mtandao wa metro.co.uk umeripoti kuwa maisha ya mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Manchester United Zlatan Ibrahimovic yameisha na ataihama timu hiyo na kuelekea nchini Marekani kucheza Ligi Kuu ya nchi hiyo MLS.
Ibrahimovic ambaye alijiunga na Man United 2016 kama mchezaji huru akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa, katika kipindi hicho akiwa Man United amefanikiwa kuifungia Man United magoli 29 katika michezo 53 wastani wa goli moja kwa mechi mbili, huku akitoa assist 9 na ameshinda mataji matatu.
Jeraha la goti la Zlatan limefanya aichezee United michezo saba pekee msimu huu na hajaichezea United toka Boxing Day katika mchezo dhidi ya Burnley iliyomalizika kwa Man United kupata sare ya kufungana magoli 2-2, taarifa rasmi inatajwa kuwa itatolewa siku zijazo lakini za chini ya kapeni zinaeleza kuwa Mourinho amempa baraka Zlatan ya kujiunga na LA Galaxy.