80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

YANGA YAPATA SIRI YA KUMALIZANA NA WAHABESHI MAPEMA

Wakiwa ndio wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia katika mashindano ya kimataifa, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema wanahitaji kupata mabao ya mapema ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inatarajia kuwakaribisha Welayta Dicha kutoka Ethiopia katika mechi ya kwanza ya mtoano itakayopigwa kati ya Aprili 7 na 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Nsajigwa alisema kuwa endapo watafanikiwa kupata mabao ya mapema katika mechi hiyo ya kwanza, itawajenga wachezaji wake na kujiamini zaidi na hatimaye kuibuka na ushindi.

Beki na nahodha huyo wa zamani wa timu hiyo, alisema kupata matokeo mazuri na kutoruhusu mpinzani kupata bao ni hatua moja nzuri na wamepanga kuhakikisha hawarudii makosa waliyofanya katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo walitolewa na Township Rollers ya Botswana.

"Tunataka mabao ya mapema na hii itatuweka katika nafasi nzuri, kikubwa tunajipanga kutumia vyema uwanja wa nyumbani kama ambavyo wenzetu wanafanikiwa, tunajua hakuna mechi nyepesi katika mashindano haya, hata kwenye Ligi Kuu Bara tunashuhudia pia matokeo ya kushangaza," alisema Nsajigwa.

Aliongeza kuwa kila hatua wanayokwenda wanahitaji kuongeza juhudi ili waweze kutimiza malengo yao ya kutinga hatua ya makundi na hatimaye fainali kwa mara ya kwanza.

Naye Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema jana kuwa kikosi chao kinatarajia kuanza mazoezi leo kwa lengo la kujiimarisha zaidi.

"Tunatarajia kuanza mazoezi kesho (leo), na baadaye tumepanga kwenda Morogoro kuweka kambi, huko tutakuwa tumetulia na mwalimu atakamilisha programu yake kama alivyopanga," alisema Saleh.

Yanga imeangukia katika mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Township Rollers, mabingwa wa Botswana kwa jumla ya mabao 2-1, ikifungwa nyumbani na kutoka suluhu ugenini.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE