80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

YANGA SC: HABARI 3 MPYA LEO JUMATATU YA MARCH 26-2018

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuendelea na mazoezi leo Jumatatu ya March 26, baada ya mapumziko ya siku kadhaa.

Wakati Yanga ikitarajiwa kuendelea na mazoezi hayo habari njema ni kuwa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma naye anatarajiwa kuanza mazoezi pamoja na kikosi hicho.

Habari hii inakuja baada ya  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, kusema kuwa taarifa alizozipata kutoka kwa Daktari wa timu, Edward Bavu, mchezaji huyo yupo fiti kuanza mazoezi Jumatatu ya leo March 26-2018.

Nyika alitoa kauli hiyo mapema baada ya Yanga kuwasili ikitokea Botswana katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers FC.

Kurejea kwa Ngoma itakuwa ni habari njema, kutokana na kuwa kwenye majeraha ya nyonga toka August, mwaka jana, tatizo ambalo lilimlazimu kukaa nje ya uwanja akiuguza maumivu hayo.

Kuelekea mazoezi hayo,  baadhi ya wachezaji ambao ni Ramadhani Kabwili, Hassani Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani na Ibrahim Ajib, watakosekana kutokana na majukumu taifa,

Wachezaji hao  watakuwa na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wakijiandaa na mchezo ujao wa kirafiki dhidi ya DR Congo March 27 mwaka huu, mchezo ambao upo kwenye kalenda ya FIFA.

Mbali na Ngoma pia mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara kwa sasa sasa hawana majeruhi yoyote, ambapo wachezaji wote waliokuwa majeruhi, kama Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko na Yohana Nkomola wamerejea kikamilifu kujifua na wenzao baada ya kumaliza program binafsi za mazoezi.

Yanga inaingia chimboni kutafuta dawa ya Singida United katika michuano ya FA, mchezo unaotarajiwa kupigwa April mosi mwaka huu, na ule wa kombe la shirikisho Barani Afrika dhidi ya Walayta Dicha ya nchini Ethiopia.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE