80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

VAR ILIVYOINUFAISHA ITALY MBELE YA ENGLAND

Ikiwa Uingereza ndio nchi iliyokuwa kinara kwenye kudai matumizi ya teknolojia kwenye mchezo wa soka na kufanikisha kuanzishwa kwa Video assistant referee (VAR) hatimaye teknolojia hiyo imewasaidia wapinzani wao.

VAR imeisaida timu ya taifa ya Italia kusawazisha bao dhidi ya England kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Wembley jijini London usiku wa kuamkia leo ambapo England ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.

Dakika ya 87 mwamuzi Deniz Aytekin alilazimika kusimamisha mechi na kwenda kutazama marudio ya tukio la mlinzi wa England anayechezea Burnley James Tarkowski aliyemwangusha Federico Chiesa wa italy ndani ya eneo la 18.

Baada ya kupata uhakika wa tukio kupitia picha za marudio, mwamuzi aliamuru mkwaju wa penalti ndipo mchezaji Lorenzo Insigne akapiga na kuisawazishia Italia na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Teknolojia hiyo inatarajiwa kutumika kuamua matukio mbalimbali yenye utata kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi, kuanzia Juni 14 hadi Julai 15-2018.

Jumla ya mataifa 32 yatachuana kuwanaia ubingwa huo, ambapo bingwa mtetezi ni Ujerumani.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE