80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

TIMU NGUMU ZINAIBORESHA TAIFA STARS: SALUM MAYANGA

Kocha Mkuu wa timu ya  Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga, amesema kuwa kucheza mechi na mataifa yaliyoendelea kunasaidia kuiboresha timu yake na anaamini itafika wakati matunda mazuri yataonekana.

Taifa Stars imetoka kupoteza mechi ya kirafiki dhidi ya Algeria na kesho inatarajia kuikaribisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mechi nyingine ya kirafiki itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Nipashe jana, Mayanga, alisema kuwa Stars inapocheza na "timu ngumu" ndio inapata nafasi ya kujiimarisha na kujijenga tofauti na awali ilipokuwa inacheza na mataifa ambayo wamepishana kiwango kidogo cha ubora.

Mayanga alisema pia anaamini mechi ya kesho dhidi ya DRC itawapa nafasi nyota wake kuendelea kujifunza kutokana na kikosi hicho kuundwa na wachezaji wanaocheza ligi mbalimbali hapa duniani.

"Kiukweli mechi hizi dhidi ya timu zilizoendelea ni nzuri na zinatujenga, wachezaji wanajifunza mengi na naamini makosa waliyokuwa wanayafanya yatapungua kupitia wanavyoona wenzao wanavyocheza, nimefurahi kupata nafasi ya kujipima na Algeria na Jumanne tutakapoikaribisha Kongo," alisema Mayanga.

Aliongeza kuwa bado wachezaji wa Tanzania wanakosa uzoefu kutokana na kukosa mechi nyingi za mashindano huku wakiwa kwenye klabu wanapambana na changamoto za ndani na nje ya uwanja.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE