80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

SINGIDA LAZIMA WAKAE: 'CANNAVARO'

Nahodha wa timu ya Young Africans yenye makazi yake mtaa wa Jangwani, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kambi ya mkoani Morogoro kuelekea mchezo wao wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya Singida United imewasaidia kuwajenga na wanaamini wataenda kufanya vizuri katika mchezo huo.

Amesema wamekuwa wakifanya mazoezi magumu na mazuri, kutokana na kuuchukulia umuhimu mkubwa mchezo huo wa hatua ya robo fainali utakaopigwa katika uwanja wa Namfua mjini Singida.

"Tumeshaanza mazoezi baada ya likizo ya juma moja, tunaendelea vizuri kabisa, tumeanza na mazoezi magumu kwa mfano leo hatujagusa kabisa mpira, mchezo wetu dhidi ya Singida tumeuchukulia kwa umuhimu sana kwa sababu usiposhinda huwezi kushiriki mashindano ya kimataifa, hivyo lazima tushinde ili tuelekee hatua inayofuata," Cannavaro amesema.

Katika hatua nyingine mshambualiaji wa kimataifa wa timu hiyo Donald Ngoma ameanza mazoezi na wenzake siku ya Jumanne baada ya kufanya mazoezi ya peke yake siku ya Jumatatu kujiandaa na mchezo wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya Singida United.

Mbali na Donald Ngoma, Mshambualiaji mwingine Amiss Joselyn Tambwe yeye bado hajaanza mazoezi ya pamoja na wenzake ambao wapo kambini Mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa April Mosi mwaka huu.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE