80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

SIMBA YATIMKIA IRINGA, WANNE WATAKAOIKOSA NJOMBE MJI HAWA HAPA

Kikosi cha Simba Sc kinatarajiwa kuondoka Jijini Dar es salaam kesho Jumamosi ya March 31  kwenda Iringa, kwa ajili ya kuweka kambi ya siku 2, katika maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji FC.

Simba SC watakuwa wageni wa Njombe Mji FC April 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Saba Saba-Njombe, huku mchezo huu ukitarajiwa kupigwa majira ya saa 16:00 jioni.

Kuelekea mchezo huo Afisa Habari wa klabu hiyo Haji Manara amesema kwamba Simba itakuwa Iringa kuanzia kesho Jumamosi hadi Jumatatu mapema itakaposafiri kwenda Njombe.

“Timu itasafiri kwenda Njombe Jumamosi hii kupitia Iringa ambako itaweka kambi hadi Jumatatu, kabla ya mechi ya Jumanne ya Aprili 3.

 “Tunaamini tutashinda inshaallah, muhimu dua na sala zenu. Mtupokee nyanda za juu kusini mwa Tanzania,”amesema Manara.

Katika mchezo huo, Simba SC itamkosa kiungo wake tegemeo wa kati, Jonas Mkude ambaye aliumia kifundo cha mguu wiki hii katika mazoezi yaliyokuwa yanafanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Jijini Dar es Salaam.

Pia itaendelea kuwakosa watatu wengine ambao ni Nahodha wake, John Bocco,  ambaye ni majeruhi pamoja na beki, Salim Mbonde na kiungo Haruna Niyonzima.

Aidha Haji Manara ameiambia nijuzehabari.co.tz kuwa wachezaji wote waliokuwa kwenye majukumu ya nchi zao tayari wamerejea na wataungana na wenzao katika safari hiyo, hao no pamoja na Juuko Mrishid na Emmanuel Okwi waliokuwa kwenye majukmu ya nchi yao ya Uganda.

Katika chati ya msimamo Simba wanaongoza ligi kwa jumla ya alama 46 sawa na Yanga wenye alama hizo wao wakiwa na michezo 21, huku Simba wakiwa na michezo 20, na kutofautishwa na magoli ya kufunga na kufugwa.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE