80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

SIMBA SC VS AL MASRY KUPIGWA SAA 18:00 JIONI VIINGILIO VYAWEKWA WAZI

Wakati Simba ikielekea kwenye mchezo wa kimataifa dhidi Al Masry Jumatano ya wiki ijayo Afisa Habari wa klabu hiyo Haji Manara aweka wazi viingilio vya mchezo huo

Haji Manara ametaja viingilio hivo leo  alipokuwa na mkutano na waaandishi wa habari Jijini Dar es salaam, mchezo unatarajiwa kupigwa Jumatano ya wiki ijayo ya March 07 kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 12 kamili jioni na sio saa 16:00 jioni kama ilivyokiwa hapo awali.

Manara ametaja viingilio hivyo kuwa, kwa mzunguko itakuwa ni Tsh 5,000/- huku VIP B ikiwa Tsh 15,000/- na VIP A ni Tsh 20,000/-

Manara ataja sababu ya kuongeza mbele muda wa kuanza mchezo huo ili kuwapa nafasi mashabiki wengi waweze kuhudhuria.

Kikosi cha Al Masry kinatarajiwa kutua nchini Kesho Jumapili ambapo kitafanya mazoezi jioni Jumatatu katika uwanja wa Taifa.

Katika mkutano hio Manara amewaomba mashabiki wao kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ili kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa kwanza na kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa kati ya Machi 16 na 17 nchini Misri.

manara amewataka mashabiki wao kusahau matokeo ya sare ya jana ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Stand United kwani mchezo wa mpira wa miguu una matokeo matatu, kufungwa, kushinda au kutoka sare.

Amesema matokeo hayo hayamaanishi kuwa Simba haitaweza kutwaa ubingwa kwa kuwa bado iko kileleni mwa msimamo wa ligi.

Amewataka mashabiki wa Simba kuacha kuumizwa na historia ya mwaka jana kwa kuwa historia zipo kwa ajili ya kuvunjwa.

"Miaka ya nyuma tumewahi kuchukua ubingwa tukitoka nafasi ya nne baada ya timu tatu zote zilizokuwa mbele yetu ikiwemo Yanga kufungwa kwenye michezo yao ya mwisho," amesema Manara.

"Hata hao Yanga wamewahi kukosa ubingwa licha ya kuongoza kwa tofauti ya alama 12 ikiwa imebaki michezo sita baada ya kupoteza michezo minne."

Manara pia amethibitisha kuwa nahodha John Bocco na mshambuliaji Emanuel Okwi walipumzishwa tu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Stand United.

Manara amesema kwa kuwa wawili hao ndio kwanza wamepona majeraha yao, benchi la ufundi liliona ni vyema kuwapa mapumziko ili waweze kuwatumia kikamilifu kwenye mchezo dhidi ya Al Masry Jumatano ijayo

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE