80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

SIMBA SC: HABARI MPYA LEO JUMATATU YA MARCH 26-2018

Kikosi cha Simba jana Jumapili ya March 25-2018, kiliendelea kujifua kwenye uwanja wa Boko Veterani Jijini Dar es salaam katika kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji April 03 mwaka huu.

Katika mazoezi hayo Simba inawakosa baadhi ya wachezaji walioko kwenye majukumu ya timu za Taifa.

Wachezaji hao ni Emanuel Okwi, Juuko
Murshid , Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Shiza Kichuya ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa.

Wachezaji hao wanatarajia kurejea kikosini mapema wiki hii baada ya michezo ya kirafiki ya mataifa yao hapo kesho.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafika na DR Congo kesho Jumanne ya March 27, huku Uganda ikitarajiwa kucheza na Malawi.

Kuelekea mchezo huo na Njombe Mji, timu ya Njombe Mji imeelezea kutoridhishwa na maamuzi ya uongozi wa TFF kwa sababu ratiba inakuwa imewabana sana.

Ratiba ya Njombe Mji iko kama unavyoona hapa chini

Stand United vs Njombe Mji (Machi 30-2018)
Kambarage Stadium
Shinyanga -FA CUP.

Njombe Mji vs Simba SC Njombe (VPL)) 3 April

Stand United vs Njombe Mji (April 8-2018)
Kambarage Stadium
Shinyanga -VPL

Mbao vs Njombe mji (Aprili 11-2018)
CCM Kirumba
Mwanza -VPL

Azam FC vs Njombe Mji (April 15-2018)
Chamazi Complex
Dar es Salaam -VPL

Baada ya ratiba hiyo, Njombe Mji itarejea nyumbani mjini Mjombe kucheza na Ndanda FC.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE