RASMI AZAM FC WAACHANA NA MUDATHIR YAHYA
Uongozi wa klabu ya Azam FC umetangaza kuwa mchezaji wake, Mudathir Yahya, yupo huru kuelekea sehemu nyingine baada ya kumaliza mkataba wake.
Afisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd Maganga, amesema mchezaji huyo kwa sasa yupo huru na kama timu nyingine ikimuhitaji, ruksa kumsajili tu.
Mudathir Yahya aliondoka Azam FC July mwaka jana na kutimkia Singida United kwa mkopo, baada ya mkataba wake wa miezi mitatu uliokuwa umesalia ndani ya Azam kumalizika.
Mudathir yuko Singida United hadi sasa katika maandalizi na wenzake kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa Aprili Mosi 2018 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Namfua-Singida.