80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

NIYONZIMA, MBONDE MAMBO SAFI SIMBA SC

Wakati Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Simba Sc wakiwa na mechi 10 mbele kabla ya msimu kuisha mambo yanaonekana kwenda sawa baada ya wachezaji wao waliokuwa majeruhi kurejea.

Katika mazoezi yanayoendelea katika uwanja wa Boko kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Njombe, beki wa kati aliyepata ajali ya pikipiki siku chache zilizopita Salim Mbonde ameanza mazoezi na wenzake.

Hata hivyo, Mbonde amekuwa akizunguka uwanja pembeni ili kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya kuungana na wenzake.

Pamoja na Mbonde, habari njema nyingine ni kuwa kiungo aliyetua Msimbazi akitoea kwa watani wao wa Jadi Yanga Sc, Haruna Niyonzima, naye ameanza mazoezi ya uwanjani.

Niyonzima alipata majeraha katika mazoezi, yaliyompelekea kusafiri hadi India ambako alipatiwa matibabu katika mguu wake, na sasa ameanza mazoezi ya uwanjani lakini kwa kuzunguka pembeni ya uwanja.

Kabla ya hapa Niyonzima alisema kuwa 'Kwa sasa anajisikia nafuu na ameanza kupewa ratiba na mwalimu pia anamini mambo yatakuwa mazuri. Kuna ‘recover’ za aina mbili kuna ya daktari na mwalimu, ya daktari tayari nimeshafanya sasa hivi nafanya ya mwalimu kwa hiyo ikiisha najiunga na timu.”taarifa kutoka mtandao wa Shafih daud

“Nimemi-miss kucheza kwa sababu muda mrefu sijacheza na watu wanajua mpira ni kazi yangu lakini siwezi kuchukua uamuzi nikasema nacheza, natakiwa kwenda na ratiba ya timu, daktari na mwalimu lakini sasa hivi nipo kwenye ratiba ya mwalimu, muda si mrefu nitarudi uwanjani.”

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE