80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

NG'OLO KANTE, MWANAFUNZI MTUNDU ANAECHOMEKEA MUDA WOTE.Na Yego Sholla

Moja ya viungo wakabaji bora kabisa duniani ndani ya miaka 3 iliopita. Huwezi ukataja orodha yako ukaacha kutaja jina la mfaransa huyu kwenye orodha hiyo. Amekuwa na athari kubwa uwanjani kwenye viwanja mbalimbali pale Uingereza na kiukweli anastahili sifa kwa kazi anayoifanya.

Msimu huu ameshuka kidogo na ni wazi yeye kukosa kuwa kwenye kiwango chake hasa kimesababisha Chelsea washindwe kutoka na karatasi safi kama walivyozoea. Kikubwa ni kwamba amekosa mtu anaeweza hasa kutengeneza muunganiko pamoja naye pale kati. Ni ukweli usiopingika kuwa kuondoka kwa Nemanja Matic kumekuwa na athari kwenye ufanisi wa Kante. Kivipi? Matic alikuwa anaweza kupandisha timu huku Kante akiwa chini lakini alikuwa akimpa msaada mkubwa kwenye kuulinda ule ukuta maarufu wa mabeki watatu pale nyuma.

Msimu huu Kante ameonekana kukosa mtu wa aina hii. Fabregas anashindwa kutoa sapoti ya kutosha kwa Kante kwenye kujihami pale katikati lakini Tiemoue Bakayoko ndio amekosa ufanisi kabisa kama kiungo. Ni mtu anaeshindwa kuunganisha matukio kama kiungo pale kati. Drinkwater ni dizaini ya Matic kabisa lakini na yeye ameshindwa kuchanganya miguu yake vizuri pale kati. Kante amekuwa akifanya kazi kubwa zaidi kwenye kujihami pale katikati hivi sasa kuliko alivyokuwa na Matic na ni wazi anaonekana kuwa ameshuka kidogo kutokana na kuonesha kuchoka kutokana na work rate yake kubwa pale kati. Hiyo ndio changamoto ambayo NG'olo hakika anakutana nayo msimu huu.

Hata hivyo nitakuwa mchoyo wa fadhila nitakapoacha kuzungumzia sifa kuu ya NG'olo Kante akiwa kama kiungo mkabaji. Linapokuja swala la nidhamu ndani na nje ya uwanja sioni mchezaji anaelifanya hilo kwa ubora kwenye nafasi yake.

NG'olo kwangu hana tofauti na mtoto mtundu anaechomekea muda wote. Hata mwalimu sio rahisi kumwadhibu. Vitendo na muonekano wa Kante ndivyo vinavyomfanya awe tofauti na viungo wakabaji wote duniani. Naheshimu sana uwezo wa watu kama kina Casemiro, Can, Xhaka, Dier lakini linapokuja swala la nidhamu ya mchezo hakuna anaelifanya hilo kwa ubora kama Kante.

Hao wengine niliowataja ni ngumu kutoka bila ya kadi uwanjani. Casemiro ni mzuri sana lakini njano huwa inamhusu sana huyo Xhaka yeye nyekundu ndio sifa yake hasa halikadhalika na Can na hata Dier na ndio maana linapokuja swala la kuigharimu timu Kante uwezekano wake ni mdogo sana. Msimu uliopita kwenye ligi alioneshwa kadi za njano takribani sita tu! Hajawahi kutolewa kwa kadi nyekundu tangu nimwone kwenye ligi.

Kante pia amekuwa na nidhamu bora hata nje. Maisha yake ni siri, anatembea na Mini Cooper ndogo kabisa, hajawahi kuonekana na demu na ni mtu mwenye aibu sana.

Miaka 6 nyuma wakati niko Uingereza nilienda kucheki muvi ya Puss in Boots. Steringi alikuwa ni paka mdogo alievaa mabuti na upanga wake. Alifanya kila aina ya balaa lakini alipovua kofia na kuyatengeneza yale macho yake hakika ilikuwa ni ngumu sana kumhukumu hata kwa kula nyama yako. Huyu ndio NG'olo Kante bwana kazi anayoifanya na muonekano wake ni Kulwa na Dotto.

Uwezo wake ni mkubwa lakini kinachomfanya awe wakipekee zaidi ni nidhamu yake hasa anapokuwa mchezoni. Huu ndio ulikuwa uti wa mgongo wa Leicester na kuuzwa kwake niliona ni kama vile waliuza nusu ya timu yao. Amartey na Ndidi wanajitahidi lakini hawafikii hata robo ya uwezo wake.

Muunganiko wake na Matic ulikuwa ndio mhimili wa Chelsea msimu uliopita. Anachohitaji Kante ni mtu anaeweza kumwondoshea mzigo alionao pale kati. Drinkwater ni wazi anaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuweza kufanya hivyo lakini kwangu Kante amekuwa ni kiungo mkabaji wa kisasa zaidi kazi chafu anakupa lakini nidhamu yake haina mfano. Hapo tu ndipo huwa Kante anawaacha wapinzani wake uwanjani Credit Haatim Abdul


No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE