80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

NEMBO YA BRAZIL INAVYOMDAI NEYMAR

Na Yego Sholla

Hakuna kitu kinachomuumiza kichwa Neymar na wafuasi wake kwa sasa kama hili jeraha la kifundo alilonalo linaloweza kumfanya ashindwe kucheza kwenye kombe la Dunia au hata ashindwe kuwa kwenye ule ubora wake hata akiweza kusimama kwenye kiti alichokalia sasa.

Kwa miaka mingi Brazil wamekuwa na "Icons" kwa maana ya wachezaji ambao ndio nyota zaidi nchini humo kwa wakati fulani. Walipita kina Pele, Ronaldinho na kwa sasa ni yeye. Namba 10 za Brazili ndio zimekuwa Icons kwenye vizazi tofauti tofauti lakini wote walipata heshima kubwa ikiwemo kushinda Kombe la Dunia na Ballon D'or.  Heshima za kuwa Nembo walikuwa nazo.

Kwa sasa Neymar ndio amebeba mzigo huo. Kwa kuanzia alihitaji kujitoa kwenye kivuli cha Lionel Messi pale Barcelona maana ni wazi huwezi kuwa mchezaji bora wa Dunia kama wewe hata sio nyota kwenye timu unayocheza. Nadhani hilo liko wazi. Hatua ya kwenda PSG imempa uhuru wa kutawala lakini kuwa pale kunamlazimu afanye mambo makubwa na ya kipekee ndio aweze kuona mikono yake ikikamata ule mpira wa dhahabu mwishoni mwa mwaka.

Kama ni rekodi na historia mbalimbali basi Ronaldo na Messi wamekuwa wakizivunja kila wiki tena kama biskuti. Na hata kwenye ligi ya Ufaransa hakuna cha ajabu ambacho angekuwa amekifanya kwa kushinda taji na makombe ya Ufaransa. Hili ni jambo ambalo PSG wamezoea kulifanya hata kabla yeye hajaenda pale na ni jambo ambalo wanatarajiwa kulifanya. Na ndio maana kipimo chake kikubwa kilikuwa ni kuisaidia klabu hiyo kushinda kombe la klabu Bingwa Ulaya pekee ndoto ambayo msimu huu ilifutika kwenye mikono ya Real Madrid.

Hilo pamoja na kutwaa ubingwa wa kombe la Dunia ndio vitu ambavyo bila shaka vitampa Neymar nafasi ya kutwaa Ballon D'or. Wakati Pele, Romario na kina Ronaldinho wanacheza, wao peke yao ndio wafalme wa vizazi vyao na hakukuwa na ushindani mkubwa wa watu wawili au zaidi kama hivi sasa. Pele alikuwa sio tu mchezaji bora wa muda wake bali inasemekana hata wa muda wote. Ronaldinho alishinda kombe la Dunia na kuisaidia sana Barcelona wakati ambao miguu ya Messi ilikuwa inatotoa kwenye soka. Namba 10 zote kubwa za Brazili tangu Ballon D'or iwe ya kidunia wamebeba tuzo hiyo, Romario, Ronaldinho Kaka na wengineo.

Tuzo hii kwao ni kama ulevi na si ajabu kila aliekuwa nembo ya nchi hiyo ameibeba. Bahati mbaya kwa Neymar ni kuwa amezaliwa kwenye kipindi ambacho vita ya soka imekuwa ni kubwa na yeye ndie namba 10 ambaye Brazil yote inamwangalia. Ushindani wa Messi na Ronaldo hauonekani kuwa na dalili ya kuisha na umri wa Neymar ni miaka 26. Na wabrazili wengi huwa wana tabia moja mbaya ambayo ni ya kuridhika mapema kwenye soka na wengi huwa wanapotea kwenye 30 zao huko.

Kuwa nembo ya Brazil kunahitaji pia na heshima za Kombe la Dunia na Ballon D'or. Pele hakuwahi kushinda Ballon D'or kwani ni tuzo iliokuwa ikitolewa Ulaya tu wakati wake ilihali yeye alicheza Brazil maisha yake yote na zaidi kwenye klabu yake ya Santos. Lakini alibeba makombe ya dunia 3 na hii imetosha kumpa heshima kubwa kwenye mioyo ya Wabrazili. Romario, Ronaldinho na Kaka walibeba kila mmoja Ballon D'or na kombe la Dunia.

Lakini presha ya kuwa nembo wa Brazil kwenye kizazi hiki imekuwa kubwa mno. Neymar amekuta ufalme una watu, isitoshe pia kuwa wa kipekee binafsi ni ngumu kwani watu wameacha alama zao ngumu tayari lakini majeraha haya yamekuja kipindi cha kukaribia kombe la Dunia. Hakuwepo wakati Brazil wanatolewa nusu fainali kwenye ardhi yao miaka 4 iliopita lakini kwa sasa anaweza kutokuwepo kabisa au asiwe tena fiti kwa ajili ya mashindano haya. Mashindano yajayo atakuwa na miaka 32 Daah! Simwoni akiingia kwenye kundi la kina Pele. Anaweza kuwa ni namba 10 atakaeekwa chini zaidi Brazil. Heshima ya tuzo ndio mwokozi wake kwa kweli Credit Haatim Abdul

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE