80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

ARGENTINA ITAMKUMBUKA MESSI PALE ATAKAPOWAAGA MAZIMA NA ITAJUTA.

Na Yego Sholla

Ryan Giggs kwa sasa ndio kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales. Ni wachache mno ambao wanaweza kumkumbuka akiwa na majoka hao akiwa kama mchezaji na wengi waliamini aliipa  umuhimu mkubwa klabu yake ya Manchester United na haonekani kuwa shujaa wa taifa hilo lakini tofauti na Yasser Arafat, Giggs anaweza kuuondosha utata huo akiwa kama kocha hivi sasa.

Yasser Arafat alikuwa ni mwanasiasa wa kipalestina aliepambana sana kutetea ardhi ya wapalestina dhidi ya Waisrael waliotaka kugawa mipaka ya nchi hiyo na kutaka kufanya makazi na kuunda nchi yao. Hii ilimfanya ashike nyadhifa kadhaa nchini humo.

Mwaka 1988, Arafat alikuja na approach mpya ambapo badala ya kupigana kuwadhibiti Waisraeli aliamua kutambua uwepo wao kwa kufikia makubaliano ya suluhisho la mataifa mawili kwa maana ya Palestina-Israeli. Aliingia kwenye makubaliano kadhaa na Waisraeli ili kumaliza tofauti zao na chama chake cha PLO. Hii ikampelekea kupokea tuzo maarufu ya Nobeli mwaka 1994. Baada ya kifo chake mwaka 2004, Wapalestina wengi wanamwona Arafat kama shujaa na mpiganaji huru aliejitoa kuwa kioo cha matarajio ya wengi. Lakini licha ya kuwaonea huruma Waisrael na kukubali mzozo wao kuisha kwa kuwapa nchi wengi wanamwona kama gaidi.

Arafat alishindwa kuuodoa huu utata lakini Ryan Giggs akiwa na majoka wa Wales hivi sasa kama kocha ana uwezo wa kufanya hivyo. Kwa muda mrefu wa soka lake Giggs amepata heshima kubwa pale Manchester United lakini mashabiki wa timu yake ya taifa wana machache ya kumkumbuka na hawamwoni kama shujaa wao na wala hakuacha kumbukumbu zozote kubwa katika ramani ya soka la nchini humo.

Giggs amepambana na kupata mafanikio makubwa akiwa na mashetani wekundu katika maisha yake ya soka na kumfanya awe ndio mchezaji aliepambwa zaidi kwenye historia ya soka la Uingereza.

Kwa sasa ni wazi hii ndio nafasi pekee ya kuuondoa utata wake na timu yake ya taifa na kuonesha kuwa anaweza kuwa shujaa wao hivi sasa akiwa kama kocha jambo aliloshindwa kulifanya kama mchezaji.

Anaweza asikumbukwe kama mchezaji lakini nyadhifa ya ukocha mkuu inampa nafasi pekee Giggs ya kuweza kuuondoa utata unaomkabili kuhusu kujitolea kwake kwa ajili ya timu ya taifa na kuwaachia kumbukumbu kama gwiji hivi sasa akiwa kama kocha.

Ni wazi kwa kipindi kirefu cha soka lake pasi na kuwa majeruhi Giggs hakuonekana kujitolea vya kutosha kwa ajili ya taifa lake kama alivyofanya kwenye ngazi ya klabu. Arafat alionekana kuifanyia makubwa Palestina japo kiuhalisia aliwasaidia sana na Waisraeli kupata taifa kwa masuluhisho mbalimbali ya mezani aliyoyafanya na serikali yao.

Leo hii Arafat hana uwezo wa kuuondoa utata huu na kuonesha kuwa alikuwa mzuri na kwa Waizraeli pia ambao wanamowna gaidi licha ya kuwatambua na kufanya makubaliano ya kuwakatia mpaka na Palestina lakini Giggs ana nafasi ya pili kuonesha kuwa anaweza na yeye kuwa gwiji na kuacha alama katika soka la Uwelshi.

Alishindwa kama mchezaji sasa ana nafasi kama kocha. Giggs alistahili kuifanyia zaidi Wales na ana nafasi hiyo sasa. Ana nafasi ya kuuondoa utata uliopo kwa wananchi wa Wales na kuwaaminisha kuwa hakuwa tu shujaa wa Manchester United bali anaweza pia kuwa mtu wa aina hiyo kwa timu yake ya taifa hivi sasa akiwa kama kocha. Pumzi zilizomnyima fursa Arafat kuondoa utata wake kwa Waizraeli ndizo hizo hizo zinampa nafasi Giggs kuuondoa utata wake yeye pale Wales kuhusiana na uwezo wake wa kujitoa kwa ajili ya taifa lake.
Credit Haatim Abdul

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE