80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

MUDATHIR YAHYA NA YANGA MAMBO YAKO HIVI, AZAM FC NAO WANENA

Baada ya mkataba wa kiungo maridadi kuisha na klabu yake ya Azam Fc, taarifa za chini chini zinaeleza kuwa mabingwa watetezi wa Tanzania Young Africans wameanza kimya kimya harakati zake za usajili kwa kumuwahi kiungo huyo Mzanzibar, Mudathir Abbas Yahya.

Kiungo huyo ambaye alitua Singida United kwa mkopo akitokea Azam FC, imeelezwa kuwa, mkataba wake na Azam ulimalizika tangu mwanzoni mwa mwezi huu huku mchezaji mwenyewe akigoma kuongeza mkataba mpya.


Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Yanga zinasema, vigogo wa timu hiyo tayari wameshazungumza na kiungo huyo, hivyo wanasubiriwa kipindi cha usajili kifike wakamilishe mchakato huo.

Wakati mchakato huo kwa upande wa Yanga ukiendelea, Azam wameibuka na kutolea ufananuzi juu ya mchezaji huyo ambaye alianza kuitumikia klabu yao kuanzia timu yao ya vijana chini ya miaka 15.

Afisa Habari wa Azam, Jaffar Idd Magandga, alisema: “Mkataba wa Azam na Mudathir umemalizika mwezi huu, hivyo kwa sasa ni mchezaji huru ambaye anaweza kuzungumza na timu yoyote ambayo anaona ina maslahi kwake.

“Kwa upande wetu tunaweza kusema Mudathir ni kijana ambaye tulikuwa naye tangu kikosi cha vijana chini ya miaka 15, mpaka amekuja kupandishwa timu ya wakubwa ambapo kwa ubora wake akajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania. Tunamtakia kila la heri popote ambapo ataelekea.”

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Nyika, amezungumzia usajili wa kiungo huyo na
kusema: “Kwa sasa tupo bize na maandalizi ya mechi yetu ijayo ya Kombe la FA, masuala ya usajili yatakuja baada ya kupokea ripoti ya mwalimu mwishoni mwa msimu.

“Hivyo, kama tukianza kuzungumzia usajili katika kipindi hichi tutakuwa tunachanganya mambo, hivyo tungojee muda wa usajili ufikie ndiyo nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia hilo.”

Yanga wanakabiliwa na michuano mitatu msimu huu, ikiwa ni kombe la shirikisho Afrika, Azam Federation Cup (ASFC) na Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL).

Kutokana na baadhi ya wachezaji wa Yanga kutokuwa na msimu mzuri baada ya kuwa na majeruhi ya muda mrefu itakuwa sahihi kama watamsajili Mudthir ambaye ataweza kuziba nafasi ya Thabani Kamsoko ambaye pamoja na umri mkuwa pia amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE