80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

MAYANGA AIKANA STARS YA JANA

Kocha wa Kikosi cha Taifa Stars, Salum Mayanga amefunguka baada ya jana kufungwa magoli manne kwa moja (4-1) na Algeria kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Algeria.

Baada ya Mchezo huo  Mayanga aliulizwa swali na mwandishi wa habari kwa nini wachezaji wengi hawana utimamu wa mwili kwa asilimia 100? na kwa nini ameita wachezaji ambao hawana Match Fitness na kuwaacha wachezaji ambao wako fit.

Mayanga akijibu kwanza amewapongeza  vijana wake kwa kupambana na hayo ndio matokeo ambayo wameyapata wanajiandaa kwa mchezo unaofuata dhidi DR Congo machi 27 jijini Dar. Kuhusu uteuzi wa kikosi cha taifa stars Mayanga amedai yeye hahusiki katika utezi wa kikosi cha Taifa Stars.

Salum Mayanga amesema
 "Kumekuwa na maneno mengi kuhusu hiki kikosi cha timu ya taifa kwanza mimi sikuwepo wakati kikosi kinateuliwa aliyeteua ni kocha msaidizi (Morroco) pamoja na kamati ya Ufundi ya TFF mimi nilikwa nje nimekuja nimekuta kikosi tayari kilichatangazwa"
Alisema Salum Mayanga kocha wa kikosi cha Taifa Stars.

Kumekuwa na Malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka wakikosoa uteuzi wa kikosi cha taifa wengine wakidai kocha wameachwa wachezaji ambapo wako fit asilimia 100 na kuwaita wachezaji ambao wametoka majeruhi na wengine wakiwa hawana timu.

Mwanzoni kikosi hicho kiliitwa kikiwa na kina nyota 23 baadae wachezaji 4 John Bocco, Farid Mussa, Thomas Ulimwengu, na Hamis Abdalah walishindwa kujiunga na kikosi hicho kwa sababu mbalimbali na kocha kuamua kuongeza wachezaji 3 ambao ni Himid Mao, Shaaban idd na Rashid Mandawa.

Mkataba wa mwaka mmoja wa Kocha Salum Mayanga umeisha tangu January 01 mwaka huu mpaka sasa Kocha Mayanga anaifundisha timu ya Taifa Stars bila mkataba wowote na shirikisho la soka Tanzania (TFF) wana mpango wa kuanzisha mchakato wa kumpata kocha mpya kutoka nje ambaye atasaidiwa na Hemed Morroco ambaye alikuwa Kocha wa kikosi cha Zanzibar Heroes.

By yossima Sitta Jr.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE