80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

MATOKEO YA ALGERIA VS TANZANIA MARCH 22-2018

Timu ya Taifa ya Algeria imeendeleza ubabe kwa Tanzania baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliopigwa nchini humo.

Mchezo huo uliokuwa kwenye kalenda ya FIFA uliishuhudia Algeria ikitawala kwa muda mwingi.

Algeria walipata goli la kuongoza mapema kwenye dakika ya 13 kupitia kwa mshambuliaji wao Baghdad aliyepokea pasi mpenyezo kutoka kwa Riyad Mahrez.

Taifa Stars ilicheza kwa kujihami zaidi na kushambulia kwa kushitukiza ilipata goli la kusawazisha kwenye dakika ya 20 baada ya mpira wa kona uliopigwa na Shiza Kichuya kutua kichwani kwa Simon Msuva na kuujaza wavuni kwa urahisi.

Mashambulizi mfululizo ya ALgeria kwenye lango la Stars yalipelekea walinzi wa Stars kufanya makosa ya mara kwa mara ambapo kwenye dakika ya 43, Shomari Kapombe alijikuta akiutumbukiza kimiani mpira wa krosi katika jitihada za kuokoa.

Kipindi cha pili ALgeria iliendelea kutawala na kujipatia mabao mengine mawili kupitia kwa Baghdad na Medjan.

Matokeo hayo yanaifanya Algeria iendeleze ubabe dhidi ya Tanzania kwani huo ni ushindi wa pili mfululizo baada ya mchezo uliopita kushinda kwa mabao 7-0 kwenye dimba hilo hilo.

Ushindi huo wa 4-1 Algeria inafikisha magoli 11-1 kwenye michezo miwili iliyoicheza dhidi ya Tanzania

Baada ya kipigo hicho Tanzania inarejea nchini kujiandaa na mchezo mwingine wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya DR Congo utakaopigwa kwenye hapa Tanzania, kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam March 27 mwaka huu.

Vikosi vilivyocheza  hapo jana Alhamisi ya March 21-2018

Tanzania: Mohamed Abdularhaman, Shomari Kapombe, Gadiel Mbaga, Abdi Banda, Kelvin Yondani, Himid Mao, Mudathir Yahya/ Rashid Mandawa, Said Ndemla/Erasto Nyoni, Mbwana Samatta, Saimon Msuva na Shiza Kichuya/Mohamed Issa 'MO Banka'.

Akiba: Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Erasto Nyoni, Abdullaziz Makame, Mohamed Issa, Ibrahim Ajib, Feisal Salum, Yahya Zayd, Shaban Idd Chilunda na Rashind Mandawa.

Algeria: 16 Faouzi Chaouchi, 6 Carl Medjani, 2 Aïssa Mandi, 10 Nabil Bentaleb, 14 Salim Boukhanchouche, 9 Sofiane Hanni, 7 Riyad Mahrez, 15 El Arabi Hilal Soudani, 21 Ramy Bensebaini, 18 Zinedine Ferhat  na 20 Baghdad Bounedjah.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE