80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

MALCOM NAHITAJI KLABU KUBWA

Na Yego Sholla

Winga wa Kibrazil anayewindwa na vilabu vya Arsenal na Tottenham, Malcom amesema kwamba anataka kusaini katika klabu kubwa barani Ulaya na kwa sasa anajifunza lugha ya Kiingereza.

Klabu ya Ufaransa, Bordeaux waligoma kumuuza winga huyo mwezi Januari licha ya kuhusishwa na Manchester United, Bayern Munich , Tottenham na Arsenal.

Malcom mwenye umri wa miaka 21 alisaini mkataba mpya ambao utadumu mpaka mwaka 2021 lakini amegusia kwamba ataondoka Bordeaux mwishoni mwa msimu kama klabu kubwa itakuja kugonga hodi.

" Nataka kucheza katika klabu Barani Ulaya , kutwaa UEFA na kucheza katika kikosi cha Selecao,"

" Pindi nikicheza kwenye klabu kubwa, nafasi yangu ya kucheza Brazil inaongezeka . Nataka kuishukuru Bordeaux kwa kila kitu.Kwanza nataka kumaliza msimu kwa matokeo mazuri iwezekanavyo baada ya hapo nitakaa chini na Familia yangu na wakala wangu."

" Pamoja tutafanya maamuzi."

Malcom anaamini kwamba ataweza kuzoea vizuri ligi ya Uingereza kama ofa kutoka huko itatua mezani.

" Najifunza Kiingereza, kwasababu ni lugha muhimu sana Duniani . Popote utakapokuwa,ukijua Kiingereza unaweza kuishi . Kwahiyo hiyo ni muhimu sana kwangu."

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE