80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

MAKALA:WALICE KARIA RAIS WA TFF NA MADUDU YA SOKA LETU PALE TFFBy Joseph michael

Baada ya kumalizika uchaguzi wa TFF pale Dodoma na kupatikana ndugu Wallace Karia kama rais na Wambura kama makamu wa rais wa TFF nilifarijika kidogo na kuamini TFF ilipata watu sahihi kwa nafasi sahihi!!

Lakini kilichotokea na kinachoendelea ni vitu viwili tofauti kwanza nikajua ndugu Karia ataacha masuala ya ushikaji kwenye utendaji lakini baada ya kuona kawateua ndugu Mgoyi na Nyamlani alinipa ukakasi kidogo na kuniacha na maswali mengi kichwani swali la kwanza iweje wawe Mgoyi na Nyamlani???

Hakuna wengine wanaofaa kuteuliwa kwenye hizo nafasi?? Jibu nikapata hawa jamaa ni marafiki na hao ndio watu waliomsaidia kuingia madarakani
Mara paaap Wilfred Kidau anateuliwa kukaimu nafasi ya katibu mkuu sikuwa na shaka na cheo ila shaka niliyoipata je kidau ana sifa za kukaimu ile nafasi na mbaya zaidi kakaimu zaidi ya miezi sita wakati kanuni za TFF haziruhusu nafasi hiyo kuteuliwa zaidi ya kutangazwa nafasi ya ukatibu mkuu na watu wenye sifa kutuma cv zao na kufanyiwa usaili kuona yupi amekidhi na kufaa kuwa katibu mkuu wa TFF lakini hili limekuwa kinyume chake!!

Mara paap suala la Wambura kufungiwa hili hapa, kwanza zilianza tetesi atafungiwa kutojihusisha na soka maisha mwanzoni nikahisi ni zile stori za mitandaoni lakini baada ya muda nikasikia kuna kikao cha kamati ya utendaji ya TFF na agenda kuu ikawa Wambura na kilichonitia ukakasi zaidi ni suala la kikao kuendeshwa kwa siri na kuviziana.

Sipo hapa kumtetea Wambura lakini nipo hapa kuongea ukweli iweje kikao kiitishwe ilihali mtuhumiwa hayupo?? Walipata wapi nafasi ya kusikiliza mshitakiwa anasemaje na anajiteteaje?? TFF wanamuogopa Wambura mpaka wamvizie??

Walipata wapi ujasiri wa kuweka hoja zao mezani na kushindwa kusubiri utetezi wa mshitakiwa?? Suala la kumfungia Nchema na Razack lilichukua zaid ya wiki mbili au tatu ilihali kulikuwa na ripoti za waamuzi na marejeo ya mechi kupitia azam tv ila suala la kuthibitishwa na sheria na vyombo vya usalama linaamuliwa kwa masaa kadhaa, kwahiyo wanataka kuniaminisha suala la Wambura lilikuwa na uharaka wa maamuzi kuliko kufungiwa kwa wachezaji??

Hatuja kaa sawa Rufaa ya Wambura inapigwa danadana hapa najiuliza kama TFF walikuwa sahihi na maamuzi yao kwanini wamzungushe Wambura kupokea rufaa yake??? Kuna nini wanachokikwepa hapa?? Blatter alifungiwa kutojihusisha na soka lakini FIFA wahajawahi kumzungusha kukataa rufaa kwa sababu FIFA wanaamini kwenye maamuzi yao na ndio maana hawana pressure na rufaa ya Blatter, drama zitaisha lini kwenye soka letu??

Mara Nyamlani ateuliwa kukaimu nafasi ya Wambura, kanuni za TFF zinasemaje mtu wa kukaimu anatakiwa awe mjumbe wa kuchaguliwa wa TFF na si wakuteuliwa ila chakushangaza ndugu Nyamlani ni mjumbe wa kuteuliwa kwahiyo ameshapoteza sifa za kukaimu nafasi yeyote ndani ta TFF, Karia amekaa kimya kwenye hili hajawahi kutamka chochote na mbaya zaid wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFF wanalalamika suala la Nyamlani lakini viongozi wa TFF hawasikiii masikio wameweka pamba!!

Halijaisha la Nyamlani linaibuka la Kidau kuwa katib mkuu wa TFF, japo mpaka sasa halijatamkwa lakini kwa mujibu wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFF ndugu Kidau ameshapitishwa kuwa katibu mkuu wa TFF kwa hisani ya ndugu Karia, hapa najiuliza kanuni gani wanayoitumia wajumbe kumpitisha ndugu Kidau kuwa katibu ilihali hii ni nafasi ya ajira na hutangazwa na si kupitishwa na wajumbe wa kamati ya utendaji?? Kidau pia ni mjumbe wa TFF kupitia TAFCA ( chama cha makocha Tanzania) ilihali kanuni za TFF zinasema Katibu wa TFF hatakiwi kuwa mjumbe wa TFF, hapa ndugu Karia inabidi atueleze ametumia kanuni gani kumbeba shawiba wakeb Kidau!!

Za kunyapianyapia zinaeleza kamati ya maadili ya TFF wajumbe wake wamebadilishwa mara baada ya ndugu Wambura kuwasilisha rufaa yake hapa haiingii akilini hata kidogo, kwanini kamati ibadilishwe wakati kuna shauri mbele yao??

Au bado wanamuogopa wambura na hawawaamini wanakamati wao??
Mara paap Mayanga asema hakuhusika na uteuzi wa timu ya taifa japo alikuja kukana lakini kiukweli Mayanga alituonesha madudu yanayoendelea pale Karume kama tim ya taifa inateuliwa na kamati ya utendaji ya TFF tutegemee nini kwenye mechi dhidi ya Algeria??

Karia tulikuwa na imani nawe ila kwa sasa mpira umekushinda na TFF imekushinda pia
Tunahitaji mpira wetu
Karia kaa pembeni kidogo
Tupishe TFF na maswahiba zako!!

Karimu Kondo
0714373232

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE