80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

KUMJIBU MTU MJINGA NI KUFANANA NAE..ILA KUMWELIMISHA MJINGA NI KUMSAIDIA (MANARA)

Toka jana kwenye kurasa za mitando ya kijamii kumekuwa kukisambaa video ya mahojiano kati ya mwandishi mwandamizi wa gazeti la Championi, Saleh Aly na beki Abdi Banda anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika klabu ya Baroka FC.

Moja ya maswali aliyoulizwa Banda na mwandishi ni aeleze kitu gani kinachomkera na katika soka la Tanzania.

Katika majibu yake Banda alisema ni kitendo cha viongozi wa soka nchini 'kulalamikia' kupinga maamuzi ya waamuzi kwa mfumo ambao yeye binafsi haukubali.

Akatolea mfano tukio la Afisa Habari wa Simba Haji Manara kuitisha Mkutano wa Waandishi wa habari kulaani klabu ya Simba kunyimwa penati kwenye michezo dhidi ya Yanga na Mbao FC. Manara aliweka ukumbini runinga kuonyesha jinsi Simba ilivyoonewa kwa kunyimwa penati kwenye michezo hiyo.

Mahojiano hayo yamemfikia Manara na amelazimika kujibu maswala ya Banda ili kuweka kumbukumbu sawa.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Manara ameadhika hivi;

Kumjibu mtu mjinga ni kufanana nae..ila kumwelimisha mjinga ni kumsaidia

Nimeona hyo video ya Saleh Ally na mchezaji wa Baroka fc (Kama nimeiandika vema )ya nchini Afrika kusini Abdi Bhanda.

Bhanda alipata kuichezea klabu ya Simba kabla ya kujisajili na timu yake mpya.

Kwenye video hyo Bhanda anaulizwa swali na mwandishi ni kitu gani hutatamani kikutokee ktk career yako ya kucheza Soka.. akajibu.jambo nisilotaka kuja kuntokea ni kwa viongozi waliopewa dhamana kuchukua mamlaka ya kwenda kuongea na vyombo vya habari huku wao hawana mamlaka hayo..huku akikiri kuwa kuna watu wameajiriwa kwa kupewa hyo mamlaka..

Halafu akaendelea kwa kuponda kwa mfano wangu eti kulalamikia maamuzi ya refarii aliochezesha mchezo wetu wa Ligi kuu baina yetu na Yanga..mchezo ulioisha kwa sare ya bila kufungana..

Mchezaji huyo alienda mbali zaidi kwa kusema jambo hilo linasababisha mpira wetu usiende mbele..

Nimjuze kwanza wajibu wa kazi yangu..mm ndio msemaji rasmi wa klabu ya Simba na nimepewa hyo mamlaka kama alivyosema yy mwenyew ktk interview yake..nikiongea mm naongea kwa niaba ya kamati ya kamati ya utendaji wa Simba..siongei jambo ila uongozi umeridhia na ndio maana kwa kipindi chote ambacho nipo Simba haijatokea hata kwa bahati mbaya mm kupishana kauli na viongozi wenzangu..
Hvyo dogo aelewe ile ni mamlaka yangu.

Pili mm kwenda kulalamikia maamuzi yale ni stand ya klabu na sikukurupuka kama alivyokurupuka yy ambae hata hajui nani msemaji rasmi wa klabu ya Simba..nimwambie kuanguka kwa mpira kuna sababu nyingi nchini na sio kulalamikia waamuzi pekee..hata huko South unapoomba Mungu watu hulalamikia waamuzi na walalamikaji ni viongozi,mashabiki,makocha na hata wachezaji.

Pia asisahau kulalamika kwangu ndio kulimsaidia asifungiwe adhabu kubwa na TFF baada ya kumpiga George kavila wa Kagera Sugar,hali iliopelekea kupata fursa ya kucheza Cosafa cup ambapo akaonekana na kusajiliwa huko South..

Nimkumbushe pia kulalamika kwangu ndio kulikopelekea utetezi ktk shauri lake kwa uongozi wa Simba ambapo alikuwa afukuzwe timu kitambo kwa kukosa nidhamu na maadili ya kambi..tena nilifanya utetezi mbele ya Bi mkubwa wake na bwana Bosnia ambae ni kama mlezi wake
Na hapo sitaki kumkumbusha huo ulalamishi wangu ulivyomnusuru yy ktk lile shauri lake la jinai..

Nimalizie kwa kumwambia weka akiba dogo..bado hujafika kokote wala usijione ushakuwa Abedi Pele au Lucas Radebe..huwa nazisikia tambo zako mbalimbali ukihojiwa na media za Tanzania..wakati mwingine ukibeza hata ulipotoka!!

Sijui ungekuwa ww ndio Samata ingekuwaje?
Sijawahi kumsikia Samata kwa njia yoyote akiponda hadharani viongozi wa bongo wala Simon Msuva au Ulimwengu..ila ww uliohamishia mpira mdomoni..jifunze kwa waliokutangulia na ujiwekee malengo yako ili ww,familia yako na Taifa kwa ujumla wafaidike,kupambana na mtu mwenye taaluma ya kuongea na kuandika ni kututafuta muhali tukaja kuongea yasioandikika....

Tazama Video hapa chini Abdi Banda alipohojiwa na Saleh Ally kuhusu kitu gani hapendi kitokee huko South Africa.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE