80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

KAULI YA NSAJIGWA KUELEKEA MCHEZO WA KIMATAIFA DHIDI YA WELAYTA DICHA YA ETHIOPIA

Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye mashindano ya kimataifa, Yanga, wameshaanza mikakati ya kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga imeanza kujifua jana kujiandaa na mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Singida United utakaopigwa kwenye uwanja wa Namfua April 01.

Baada ya mchezo huo Yanga itarejea uwanja wa Taifa kuivaa Welayta kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano kombe la Shirikisho kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi, April 07.

Yanga itawafuata wapinzani wao kwa ajili ya mechi ya marudiano ya hatua hiyo ya mtoano  Aprili 17 huko Addis Ababa, Ethiopia.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema ili wawe na uhakika wa kusonga mbele ni lazima wahakikishe wanapata matokeo mazuri katika uwanja wa nyumbani na hawataki kuona wanarudia makosa waliyofanya kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.<

Nsajigwa amesema changamoto waliyokuwa nayo ni kujiandaa vyema kwa ajili ya mechi hiyo huku vile vile wakitakiwa kupambana ili kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanaoushikilia.

"Kama nilivyosema jana (juzi), fainali yetu, hesabu zetu tunatakiwa kuzifunga hapa nyumbani, unapofanya vizuri nyumbani au katika mechi ya kwanza, unajiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele, hiyo ndiyo siri ya mafanikio," alisema Nsajigwa.

Yanga imehamia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na mabingwa wa Botswana, Township Rollers kwa kichapo cha mabao 2-1 walichofungwa hapa nyumbani wakati Welayta Dicha yenyewe imeiondoa Zamalek ya Misri kwa penalti 4-3 baada ya kufungana mabao 3-3.

Wapinzani hao wa Yanga ambao ni mabingwa wa Kombe la FA huko Ethiopia mwaka jana, wako katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ya ndani wakiwa na pointi 19 baada ya kushinda mechi tano na kutoka sare michezo minne wakati vinara ni Dedebit wenye pointi 29.

Mshindi wa jumla kati ya Yanga na Welayta Dicha atatinga hatua ya makundi ya mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Mara ya mwisho Yanga kutinga hatua ya makundi ilikuwa ni mwaka 2016, walipopangwa kundi moja na Medeama ya Ghana, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mo Bejaia ya Algeria.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE