80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

KAULI YA KOCHA MSAIDIZI, SIMBA IKIANZA KUIWINDA NJOMBE MJI

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema watautumia vyema muda ambao timu hiyo haina mechi za kimataifa na Kombe la FA kurekebisha makosa ya kiufundi waliyoyabaini ili warejee kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na kasi.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza mazoezi leo Jumamosi ya March 24-2018, kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao dhidi ya Njombe Mji FC itakayopigwa Aprili 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Saba Saba mkoani Njombe.

Djuma, amesema wanataka kuona hawapotezi pointi katika mechi zao zote zilizobaki ili kutimiza mipango yao ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

Djuma amesema wana lengo la kukiimarisha zaidi kikosi chao kwa sababu hatua iliyobaki ni ngumu zaidi kutokana na vita ya kuwania ubingwa na ile ya kushuka daraja kufanana.

"Tunaelekea mwisho wa ligi, huku ni kugumu zaidi na ndio tunahitaji kushinda, ukipoteza pointi, basi umempa nafasi mpinzani wako, hatutaki kuona tunapoteza hii nafasi iliyobaki ya kushinda taji msimu huu,".

Djuma aliongeza kuwa mechi zote zilizobaki kwenye ligi ni ngumu na wanawakumbusha wachezaji wao kutobweteka au kuingia uwanjani na matokeo ya mzunguko wa kwanza.

Simba imayonolewa na kocha Mfaransa kimerejea kwenye Ligi Kuu kamili baada ya kuondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Al Masry ya Misri ambayo ililazimisha sare ya mabao 2-2 walipokutana March 7 mwaka huu Jijini Dar es Salaam na kutoka sare ya bila kufungana nchini Misri.

Katika chati ya msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara yenye timu 16 Simba inaongoza kwa jumla ya alama 46, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana pointi 46, lakini wakizidiwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, huku Azam FC wenye pointi 43 wakiwa katika nafasi ya tatu.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE