80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

KAGERA SUGAR, NJOMBE MJI, AZAM FC MAMBO SAFI, TZ PRISONS VS MBAO KUPIGWA LEO

Timu ya Kagera Sugar imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Maji Maji ya Songea katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba-Bukoba.

Hadi mpira unaenda mapumziko, Kagera Sugar walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliajiwa zamani wa Simba SC, Christopher Edward Shijja katika dakika ya 35.

Majimaji walisawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga Jerson ‘Jerry’ ’John Tegete, dakika 5 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Wenyeji, Kagera Sugar wakafunguka kufanya mashambulizi ya nguvu kusaka bao la jingine na wakafanikiwa katika dakika ya 72, ambapo Japhet Makalai aliweza kuipatia Kagera Sugar bao la 2.

Matokeo hayo yanairudisha Maji Maji nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, mbele ya Njombe Mji zote zote zikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 20, wakati Maji Maji sasa ndiyo inashika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 20 pia.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu kati ya wenyeji, Tanzania Prisons na Mbao FC ya Mwanza ulihairishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika Mji Mbeya.

Mchezo mwingine uliochezwa mapema ulikuwa kati ya Njombe Mji vs Ruvu Shooting, ambapo Njombe waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Njombe Mji yalifungwa na Ditram Nchimbi katika dakika ya 27 na Jimmy Mwaisondola kwenye dakika ya 56, huku la kufutia machozi ya Ruvu Shooting likifungwa na Baraka Mtuwi katika dakika ya 32.

Mchezo wa mwisho ulizikutanisha Azam Fc ya Dar es salaam dhidi ya Singida United ya Singida ambapo Azam Fc walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao la Joseph Mahundi katika dakika ya 16.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE