80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

HIKI NDICHO KIASI ANACHOKATWA MCHEZAJI WA SIMBA ANAYECHELEWA KULA

Uongozi wa benchi la ufundi la Simba umeweka sheria kali ambapo kila mchezaji akichelewa kwenye matukio maalum anakatwa shilingi laki moja.

Uongozi huo chini ya kocha Pierre Lechantre umeweka sheria hiyo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa timu hiyo inakuwa na nidhamu ya hali ya juu.

Sheria hiyo ya Simba inasema kuwa kama mchezaji akichelewa kula, akichelewa mazoezini, akichelewa kwenye basi na sehemu nyingine muhimu anakatwa kiwango hicho cha fedha.

“Huu ni utaratibu wetu kwa muda mrefu kidogo kuanzia benchi hili la ufundi limeanza kazi.
“Wachezaji wanatakiwa kuwahi sehemu zote muhimu, kila sehemu hata Ulaya wachezaji wanatakiwa kula pamoja, wanatakiwa kuwahi kwenye basi na mazoezini.

“Utaratibu huu umeleta nidhamu ya hali ya juu klabuni, ndiyo maana umeona timu inafanikiwa kwa sasa kwa kuwa kuna nidhamu ya hali ya juu sana kwa sasa.

“Kama kwenye chakula na sehemu nyingine kocha ndiye amekuwa akimwita meneja na kumwambia mkate mchezaji fulani shilingi 100,000, hii ni faida kubwa kwetu,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya klabu hiyo.

Hata hivyo, kuanzia utaratibu huo umeanzishwa inaelezwa kuwa mchezaji anayeongooza kwa nidhamu ni Shiza Kichuya.

Championi

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE