80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

DAVID DE GEA, PEPE REINA NA MARC-ANDRE WAKOSOA VIKALI MPIRA UTAKAO TUMIKA KOMBE LA DUNIA

Na Yego Sholla

Mpira ambao utatumika kwenye fainali za kombe la Dunia nchini Urusi umekosolewa sana kutoka kwa Magolikipa  David de Gea, Pepe Reina na Marc-André ter Stegen.

Baada ya kutumika kwa mara ya kwanza mwezi Novemba mwaka Jana , Adidas Telstar 18 umebuniwa tena kutoka kwenye mpira uliotumika kwenye fainali za kombe la Dunia za mwaka 1970 na 1974, na ulitumika siku ya Ijumaa ambapo taifa la De Gea na Reina lilipotoka sare dhidi ya Ujerumani ya Ter Stegen.

" Mpira unafanya vitu vya ajabu , mwendo wake na upaaji wake hautabiriki na bado kuna chumba kikubwa sana cha kuboresha." Wamesema magolikipa hao wote watatu.

" Nakutabiria mimi tutashuhudia angalau magoli 35 kutoka umbali mrefu Urusi , kwasababu haiwezekani kuutabiri upaaji wake:" Amesema Reina. " Umezungushiwa na plastiki na kufanya kuwa ngumu kuudaka."

" Magolikipa watakuwa na matatizo mengi sana na huu mpira, ni wa ajabu sana." Amesema De Gea ambaye alikuwa golini katika dimba la Esprit Arena kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Ujerumani, akifungwa goli na Thomas Müller kwa shuti kali kutoka nje ya boksi . " Ungeweza kutengenezwa vizuri zaidi."

Ter Stegen ambaye naye alicheza mechi hiyo  amesema," Mpira ungeweza kuboresha zaidi. Unayumba sana, lakini nafikiri itabidi tuufanyie sana mazoezi na tuuzoee mapema sana kabla ya Kombe la Dunia "

" Hatuna chaguo lingine."

Hata hivyo Reina ametofautiana na Ter Stegen " Inabidi waubadilishe , bado kuna muda wa kutosha."

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE