80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

DAKTARI YANGA AZUNGUMZIA HALI YA DONALD NGOMA KWA SASA

Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu amemruhusu mshambuliaji wao Donald Ngoma kucheza dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia kwa kumuanzishia programu ya kuuchezea mpira kama sehemu ya maandalizi ya mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ngoma amerejea uwanjani akitokea kwenye majeraha ya nyonga aliyoyapata tangu Agosti, mwaka jana kutokana na tatizo hilo na kulazimika kukaa nje ya uwanja akiuguza maumivu hayo.

Yanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika inavaana na Wolayta baada ya droo kuchezeshwa na mchezo wa kwanza utapigwa Aprili 7 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Bavu alisema Ngoma ataanza mazoezi hayo ya kuchezea mpira baada ya kumaliza programu ya mazoezi ya binafsi ya peke yake ya kukimbia mbio fupi na ndefu.

Bavu alisema, mshambuliaji huyo tayari amemaliza programu hiyo na Jumatatu ijayo asubuhi ataanza mazoezi magumu na wenzake ikiwemo kuchezea mpira akijiandaa na mchezo wa kimataifa.

“Kila mazoezi aliyokuwa akiyafanya Ngoma yalikuwa na programu yake na tayari amemaliza programu yake ya mazoezi ya binafsi ya kukimbia mbio fupi na ndefu baada ya kumzuia kuchezea mpira.

“Hivi sasa tayari amemaliza programu hizo na Jumatatu ataanza programu ya kuchezea mpira pamoja na wenzake katika mazoezi ya kujiandaa na mechi na Waethiopia.

“Nilimpa programu hizo baada ya kuhofia kujitonesha kama unavyojua ametoka kwenye majeraha makubwa na alikaa nje muda mrefu ni lazima aanze taratibu,” alisema Bavu.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE