80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

CARLOS CARVAJAL :MOURINHO NI BORA ANAPOPIGANA NA WATU

Na Yego Sholla

Kocha wa Swansea, Carlos Carvalhal amesema kwamba kocha wa Manchester United Jose Mourinho huwa anastawi zaidi " Pindi anapopigana " na watu.

Makocha hao wawili watakabiliana siku ya Jumamosi katika dimba la Old Trafford kwenye mechi ya EPL ambapo Swansea wakiwa wanasaka pointi muhimu za kujinusuru kushuka daraja.

Carvalhal, ambaye aliwahi kutumia muda kujifunza chini ya Jose Mourinho pale Chelsea amekiri kwamba kuna baadhi ya vitu wanafanana na Mourinho lakini amesema kocha huyo wa zamani wa Inter Milan na Real Madrid anapenda mbinu za malumbano.

" Nampenda Mourinho na anajua kwamba nampenda. Nimemsoma sana. Nilitumia wiki nzima Manchester United pindi  Alex Ferguson alipokuwa pale. Halafu wiki tena pindi Mourinho alipokuwa Chelsea , na alipokuwa Real Madrid."

" Nilijaribu kujifunza kutoka kwa makocha bora. Anajiamini sana. Kama mimi . Na unahitaji hiyo. Lakini yupo tofauti na mimi kiutu.Anapenda Malumbano. Anapenda kupigana an watu . Na huwa anakuwa bora sana pindi anapopigana na watu."

" Mimi nipo tofauti kabisa. Napenda kuwa mbali sana na malumbano . Napenda kushinda, lakini kama mtu akijaribu kupigana na mimi, basi watajikuta wanapigana wenyewe."

" Kama klabu siku moja ikinifukuza , asubuhi inayofuata , nitawaonea huruma kwasababu watakuwa wamepoteza kocha mzuri sana."

" Nina ujuzi mzuri. Kwa nadharia na vitendo. Najua kwamba nina uzoefu na nipo tayari kwa kila kitu."

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE