80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

BAYERN MUNICH NA SILAHA ROBERT LEWANDOWSKI KATIKA NJIA ZA ALEXANDER THE GREAT.I Na Yego Sholla

Kati ya mwaka 336–323 kabla ya kuzaliwa Kristo, utawala na nchi ya Macedonia ulikua mkubwa sana. Chini ya Uongozi wa Kijana mmoja mtoto wa Mfalme Filippo II wa Macedonia na malkia Olympias Macedonia, Alexander The Great. Huyu alikua kiongozi, mtawala, mfalme na amri jeshi mkuu wa tawala yote ya Macedonia, Nchi iliyokua kaskazini wa Ugiriki ya kale.

Alexander The Great anatajwa kama amri jeshi mkuu mashuhuri zaidi kuliko wote kwenye historia ya dunia. Huyu alianza kutawala himaya ya Macedonia mwaka 336 KK wakati huo akiwa na umri wa miaka 20 Tu mara baada ya baba yake Mfalme Filippo II kufariki kwa kuuwawa na mmoja kati ya walinzi wake.

Mara baada ya kukalia kiti cha ufalme kazi ya Alexander The Great ilikua ni kuendeleza kile alichokianza baba yake kwa kuongeza zaidi himaya ya utawala wake. Akiwa kama kiongozi na amri jeshi mkuu, Alexander The Great alipambana vita nyingi ili kuhakikisha anashinda na kutawala sehemu kubwa ya dunia kuanzia Ulaya hadi Bara Hindi na Misri.

Historia inasema Alexander The Great hakuwahi kushindwa kwenye vita. Kila vita aliyopambana alishinda. Hii ilifanya utawala wa Macedonia uwe mkubwa sana. Alifariki akiwa na miaka 33. Inatajwa kwamba kama Alexander The Great angeendelea kuishi kwa miaka mingi basi utawala wake ungekua mkubwa zaidi hadi sehemu za China na Afrika.

Club ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani inapita katika hatua za utawala wa Macedonia enzi hizo. Tofauti na himaya ya Macedonia iliyokua chini ya kiongozi na amri jeshi mkuu Alexander The Great, Bayern Munich ipo chini ya uongozi wa Robert Lewandowski mwenye kazi moja Tu, kazi ya kufunga magoli.

Bayern Munich wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitawala ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga kwa muda mrefu sasa. Tangu mwaka 2012 wameshinda ubingwa wa bundesliga kwa misimu mitano mfululizo. Msimu huu wanaweza kutwaa tena na kufanya iwe jumla ya misimu sita mfululizo.

Si wakati huu pekee, Tangu mwanzo na misimu mingi iliyopita Bayern Munich imekua ikilitawala soka la Ujerumani kwa kiasi kikubwa wanafanya kila wanachokitaka. Wameshinda jumla ya mataji 26 ya Bundesliga, wanaofutia kwenye orodha ni Borussia Mönchengladbach na Borussia Dortmund walioshinda mara 5 kila mmoja. Ajabu kweli Hii!!

Tangu enzi za kina Gerd Muller, mfungaji bora wa muda wote wa Bundesliga hadi kwenye utawala wa Robert Lewandowski, Bayern Munich imeendelea kua papa kwenye soka la Ujerumani ikivimeza vilabu vingine. Faida kubwa kwenye uwekezeji na udhamini mkubwa inaoupata Bayern Munich imewapa nguvu kubwa ya kuendelea kufanya kila wanachokitaka.

Kama ilivyokua kwenye utawala wa Alexander The Great na Macedonia yake alivyokua akiteka kila tawala na kulimiki, Bayern Munich nao wamekua wakisajili kila mchezaji bora anayecheza Bundesliga. Kwa miaka ya hivi karibuni Michael Ballack, Miroslav Klose, Lukas Podolski, Ivica Olic, Mario Gomez, Mario Mandzukic, Mario Gotze, Roberto Lewandowski, Nicklas Sule, Manuel Neur, Matts Hummels, Sebastian Rudy, Serge Gnabry na Leon Goretzka wote wamesajiliwa wakiwa wachezaji wazuri na tegemeo kwenye club zao.

Hata wachezaji wengi wa Kijerumani wanaonekana hawajakamilika zaidi kama hawajapata nafasi ya kuichezea Bayern Munich. Wachezaji wengi wa Kijerumani wanapenda kuichezea Bayern Munich. Franz Beckenbauer, Karl-Heinz Rummenigge, Gerd Muller, Oliver Khan, Lothar Matthaus, Hans-Georg Schwarzenbeck, Jürgen Klinsmann, Phillip Lahm, Bastian Schwainsteiger na Michael Ballack ni baadhi ya wachezaji wanaoheshimika sana nchini Ujerumani hawa wote wameicheza Bayern Munich kwa vipindi tofauti.

Bayern Munich ipo chini ya Robert Lewandowski kwa sasa, mshambuliaji anayefunga kadiri anavyotaka. Mpaka sasa Bayern Munich inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 17 mbele  ya Shalke 04 anayekamata nafasi ya pili. Huku Robert Lewandowski akiongoza orodha ya wafungaji akiwa na magoli 23 huku Pierre-Emerik Aubameyang ambaye sasa hayupo nchini Ujerumani na Nils Petersen wa Freiburg wakimfuata wakiwa na magoli 13 kila mmoja.

Bora angekuwepo Aubameyang huyu Petersen hana uwezo mkubwa wa kushindana na Lewandowki kwenye tuzo ya mfungaji bora. Mwisho mwa msimu iko wazi kwamba Bayern Munich atatwaa ubingwa huku Robert Lewandowski akitwaa tuzo ya mfungaji bora.

Kama mambo yataendelea kuwa hivi basi kwa miaka mingi ijayo tutaendelea kuishuhudia Bayern Munich ikitawala soka la Ujerumani kila msimu. Tena watakua wanatangaza ubingwa mwezi March au April kama ilivyokua kwenye misimu iliyopita. Ubora wa ligi ya Ujerumani unapotea. Mvuto unapotea pia. Hii imesababisha hata kwenye mashindano ya Ulaya ni Bayern Munich pekee inayoonekana kufanya vizuri kwa kufika hatua za mbali. Msimu huu Borussia Dortmund walishindwa kufuzu hatua ya makundi UEFA Champions League, hata kwenye Europa League wameshindwa kufika hatua ya robo fainali. Timu nyingi za Ujerumani hazifanyi vizuri kwenye mashindano ya Ulaya.

Nadhani kuna uhitaji wa kufanya uwekezaji mkubwa sana kwenye Bundesliga hasa uwekezaji kwenye hizi club zinazoonekana kuwa za kawaida. Mpira siku hizi umekua ukiendeshwa kwa pesa. Club nyingi za Ujerumani bado hazijapata udhamini mkubwa kama wanaoupata Bayern Munich. Bado hazijawa na jeuri ya kufanya usajili wa £50M kama wanaoufanya Bayern Munich. Hii imesababisha kuruhusu wachezaji wao mastaa kuondoka.

Hakuna namna nyingine inayoweza kufanyika ili kurudisha ushindani kwenye Bundesliga zaidi ya kuzipa udhamini mkubwa hizi timu za kawaida. Vinginevyo tutaendelea kuona Bayern Munich akiendelea kutawala soka la Ujerumani kadiri anavyotaka kama vile Alexander The Great alivyokua anatawala himaya yake ya Macedonia kwa kutawala kila sehemu aliyoitaka.credit Tom Thomas

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE