80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

AZAM FC YAMPIGA MTU 5G MECHI YA KIRAFIKI

Klabu ya Azam FC, imeichapa Friends Ranger mabao 5-0 katika mchezo wa kirafiki uliomalizika usiku wa jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa ni maalum kwa ajili ya wachezaji wa Azam FC kupata mechi ya ushindani kufuatia kusimama kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kupisha mechi za kirafiki zilizo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Vilevile benchi la ufundi la Azam FC limeutumia mchezo huo kama sehemu ya kupasha misuli kuelekea mtanange wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Machi 31 mwaka huu saa 19.00 usiku.

Azam FC ilianza vema mchezo huo na kujipatia bao la uongozi dakika ya nne tu, lililofungwa na winga Enock Atta kwa mkwaju wa penalti kufuatia Idd Kipagwile kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Uzembe wa safu ya ulinzi ya Friends uliinufaisha tena Azam FC dakika ya 40 baada ya mshambuliaji Mbaraka Yusuph, kuipatia bao la pili na kufanya timu yake iende mapumziko ikiwa na uongozi wa mabao hayo mawili.

Kipindi cha pili ilishuhudiwa winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga, akiingia uwanjani dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Mbaraka, ikiwa ni mechi yake ya kwanza msimu huu baada ya kupata majeraha ya goti wakati timu hiyo ikijiandaa kucheza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Ndanda mkoani Mtwara.

Dakika ya 73 kiungo Salmin Hoza, alitumia jitihada binafsi na kuipatia bao la tatu Azam FC kwa shuti la umbali wa takribani mita 30 lililomshinda kipa wa Friends, Ndugu Juma.

Kimwaga aliyeingia na moto katika kipindi hicho ukiwa ni mchezo wake wa kwanza, alihitimisha ushindi mnono wa Azam FC kwa kufunga mabao mawili dakika ya 75 na 82 huku akishangiliwa na mashabiki waliohudhuria mtanange huo.

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kinatarajia kupumzika kesho Jumapili kabla ya kurejea mazoezini Jumatatu ijayo jioni kumalizia maandalizi ya kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo muhimu kabisa.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE