80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

ARSENE WENGER TATIZO UMRI WANGU

Na Yego Sholla

Arsene Wenger amesema kwamba baadhi ya ukosoaji anaoupata akiwa kocha wa Arsenal ni kwasababu ya ubaguzi wa umri.

Wenger mwenye umri wa miaka 68 amekabiliwa na sauti nyingi za yeye kung'atuka baada ya kushindwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu huu , na pia kukosa taji la EPL kwa muda wa miaka 14.

Lakini Wenger anaamini kwamba ukosaji wa mafanikio uwanjani huenda sio sababu pekee ya ukosoaji anaoupata ,ameiambia BeIN Sport:

" Pindi umri unaposogea, huwa unafikiria zaidi kufanya vizuri kwa klabu yako tu na kupuuzia mengineyo yote. Na unapozidi kuwa mkubwa zaidi kiumri , ndio inazidi kuwa ubaguzi wa umri ."

" Nakubali kama matokeo yanakuwa sio mazuri lazima ukabiliane na matokeo yake. lakini kiujumla ukiwa unakosolewa kwa eti muda gani nimekuwa klabuni, una umri wa miaka mingapi, hiyo inakuwa ngumu kukubali."

" Lakini mengine yote lazima nikubali , nipo kwenye kazi ya hadharani na lazima nipate matokeo na lazima nikubali nitahukumiwa kwa matokeo."

Wenger ametwaa mataji matatu ya ligi kuu ya soka ya Uingereza na mataji saba ya kombe la FA katika kipindi chake cha miaka 22 ndani ya Arsenal na anaamini kwamba pindi akiondoka klabuni , mashabiki watamkumbuka kwa yale aliyoyafanya klabuni.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE