80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

ARGENTINA ITAMKUMBUKA MESSI PALE ATAKAPOWAAGA MAZIMA NA ITAJUTA.Na Yego Sholla

Wananchi wa Argentina na wapenzi wa soka wanapaswa kufahamu kuwa kufanikiwa kwa Argentina ni zaidi ya Leo Messi peke yake kufanya uchawi wake dimbani bali na hawa wengine ni lazima wajiongeze. kiukweli inasikitisha.

Kwa sasa ni wazi kikosi kizima cha Argentina kimejivisha sura ya Messi. Wakifanya vizuri huwa ndio anasifiwa zaidi na ukweli ni kwamba hata mengi mazuri huwa yanaanzia kwake kwani wenzake hawana makubwa wayafanyayo. Lakini mabaya yamekuwa mengi na ndio yanafanya Messi asipewe heshima ya kutosha timu ya taifa na ni hawa hawa wasiojitoa pindi mwenzao akifanya vizuri ndio huwa wanamwangusha zaidi hata anapoonesha jitihada zake mambo yakiwa mabaya.

Na hapa ndio naanza kuhisi wananchi wa Argentina wamekuwa ni wanafiki tu juu ya hili mpaka nashindwa kuelewa je kwao Messi ni kama Yesu au wanamwona msaliti tu kama Yuda?

Kwa huu usaliti mkubwa unaofanywa na hawa wachezaji wengine basi wataamini kuwa Messi ni bahati kuwa naye kwenye timu hii ya taifa. Bado najiuliza wangekuwa wapi bila yeye. Kama sio mabao yake 3 ya uwezo binafsi dhidi ya Ecuador, Argentina wangeishia kulisikia tu hilo kombe la Dunia

Najaribu kuiangalia Argentina bila ya Messi. Kiuhalisia wanaonekana kuwa kwenye hali mbaya sana lakini kwani bila yeye hakuna Argentina?

Kwa uwezo walionao wachezaji wanaounda kikosi hicho hili ni jambo la kijinga kulifikiri. Ukiwafuatilia vizuri utagundua kuwa wengi wanafanya vema kwenye vilabu vyao lakini timu ya taifa wameshindwa kujitolea vya kutosha. Sijawahi kuona jitihada ya Higuian, Di Maria wala Aguero kwenye timu ya taifa lakini kwenye vilabu ni moto.

Messi anapaswa kuheshimiwa sana laiti angepata kundi la wachezaji wa wastani tu wenye ari kama ya kupambana binafsi naamini Argentina yote ingemheshimu Messi akiwa uwanjani na hata asingeonekana kama pengo wala kisingizio hata pale ambapo angekosekana kwani hao wengine wangekuwa na juhudi za makusudi tofauti na kina Higuain. Yani kirahisi tu eti kukosekana kwa Messi kuwe ni shida kwao kupata matokeo. Hatujiulizi ubovu wa Rojo, Le Celso na Higuain. Lakini shida ya Waargentina ni kwamba hata akiwepo bado watu hawaoni kama ana msaada na akikosekana pengo lake eti ndio huwa linaonekana. Waargentina wanatakiwa kumshukuru sana mungu kuwa wana Messi kwenye timu yao.

Mwaka juzi walijazana barabarani kumwomba asijiuzulu lakini ukiangalia hata kabla ya hapo ndio hao hao walikuwa wakisema kuwa hajitumi vya kutosha. Walimhitaji kwa kipi kama mchango wake hawakuuthamini?

Mkitaka kuamini kuwa Argentina hii ya kina Banega na Aguero sio riziki muondoe Messi na waende hivyo hivyo kombe la Dunia ndio utaona hata aibu kuwaangalia lakini bado hata anapokuwepo wanashindwa kumpa heshima kwa yale anayowafanyia.

Amewapeleka kombe la Dunia pale matumaini yote yalipokuwa yameisha, Aliwasaidia kufika fainali akiwa mchezaji bora wa mashindano hayo nchini Brazil. Ndio mchezaji aliekuwa na mchango mkubwa zaidi offensively kwenye Copa America mwaka juzi kikosini humo. Pengine waargentina wakikaa chini na kutafakari haya na kujiangalia walipolialia mabarabarani huko Buenos Aires ndio wanaweza kumwona Messi kama mwokozi na sio msaliti kabisa.

Baada ya kupigwa bao 6 wengi wakahisi kukosekana kwa La Pulga kulichangia. Lakini kama angekuwepo basi ndio aibu yote ingemshukia. Eeh hivi hayupo na yeye amewekwa kama sababu sikwambii angecheza. Kuna wakati huwa naamini Messi anawapima wenzake kwa majeraha haya na anaweza kuwa ana maswali mengi yaliyokosa majibu.

Inaweza kuwa ni mechi ya kirafiki lakini kwa timu kama Argentina hichi ni kipigo kikubwa mno. Kina Di Maria na Higuain wana majibu ya kutupa kwa kushindwa kumbeba mwenzao ambaye ni wazi kabisa amekuwa akizoa sana matapishi yao Credit Haatim Abdul

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE