80%

Kwa sasa tunapatikana kupitia www.nijuzehabarionline.com bofya kama haikupeleki kiautomatiki.

Your Trialversion has expired please purchase for unlimited plan.
Copyright ©

Facebook

Follow by Email

LIVE TRAFFIC STATS

Gallery

Featured Posts

Videos

Recent Posts

Recent in Sports

Column Right

Feat

Carousel

Column Left

Featured

Breaking News

ABDI BANDA ALIVYOMCHOKONOA HAJI MANARA

Beki wa zamani wa Simba Abdi Hassaj Banda ambaye sasa anachezea klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini amemtolea uvivu msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara kuwa hana weledi na kazi yake.

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo Banda akifanya mahojiano na mwandishi mwandamizi wa gazeti la Championi, Saleh Aly, ameponda tukio la Manara kuita waandishi akiwa na runginga ili awaonyeshe jinsi Simba walivyonyimwa penati kwenye mchezo dhidi ya Yanga

Banda amesema mambo kama hayo yanachangia soka letu kutosonga mbele.

"Kiongozi anaitisha mkutano na waandishi wa habari anazungumzia penati, sasa mpira utaendeleaje?," alihoji Banda.

"Badala kueleza mnajipanga vipi kwa michezo inayofuata kiongozi unabaki kulaumu maamuzi ya waamuzi wakati wote."

Baada ya kukosa ubingwa kwa misimu mitano sasa viongozi wa Simba wamekuwa wakitumia kila mbinu kujiweka kando na lawama za mashabiki wao.

Msimu uliopita viongozi hao waliwaaminisha mashabiki kuwa watatwaa ubingwa lakini waliposhindwa, kwanza wakagoma kuchukua medali za ushindi wa pili, halafu wakawaeleza mashabiki wao kuwa wamekata rufaa FIFA, wanasubiri majibu.

Lakini mpaka leo hawajawaeleza mashabiki wao nini kiliamuliwa na FIFA japo inafahamika kuwa rufaa hiyo ilitupiliwa mbali siku tatu tu tangu ipokelewe.

Msimu huu pia waliuanza kwa kutamba kuwa na kikosi ghali zaidi na hawatarudia makosa ya msimu uliopita, ubingwa kwao ni lazima.

Sasa baada ya kubaini inawezekana wakaukosa tena ubingwa, tayari viongozi hao wameanza kutumia mbinu ileile ya msimu uliopita ya kuwaandaa mashabiki wao ikitokea hawatachukua ubingwa.

Kwa nchi zinazofuata ipasavyo sheria za soka, Afisa wa Klabu hawezi kutisha mkutano na waandishi wa Habari akiwa na runinga kukosoa hadharani maamuzi ya michezo iliyopita.

Matukio ya aina hiyo ya kuwaaminisha mashabiki kuwa timu yao inaonewa yanaweza kuchochea mashabiki wakafanya vurugu viwanjani.

No comments

Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Total Pageviews

Blog Archive

Blog Rafiki

Breaking

NIJUZEHABARI ONLINE