Breaking

USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE

Saturday, March 17, 2018

2:56:00 PM

DOWNLOAD APP HII KUTAZAMA LIVE MECHI YA AL MASRY VS SIMBA SC

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Habari njema leo kwa wapenzi na wadau wa soka hapa Tanzania Nijuzehabari.co.tz itakuletea live michezo hii ifika muda wa mechi husika.

Angalia live Mechi za AL MASRY VS SIMBA SC saa 20:30 usiku huku ya  YANGA VS TOWNSHIP ROLLERS ikianza saa 16:45 Jioni

Mechi Hizi zitarushwa Live hapa hapa nijuzehabari.co.tz kwa njia ya live na live updates

Hivyo unachotakiwa kufanya kudownload app yetu ya nijuzehabari mapemaaa kwa kubofya HAPA ili kuweza kutazama live

Utaweza kupokea ujumbe wa sauti (notification) kwenye simu yako hivo utaifungua na kuanza kuangalia live ifikapo muda wa mechu hizo

Unaweza kubfoya HAPA pia kudownload app hii kwa urahisi


1:44:00 PM

HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS (LIGI YA MABINGWA)

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Kikosi cha kwanza cha Yanga dhidi ya Township Rollers saa 16:45 jioni, nijuzehabari itakuletea live updates ya mchezo huu kwa dakika 90 zote
1:Youthe Rostand
2:Juma Abdul
3:Gadiel Michael
4:Andrew Vicent
5:Kelvin Yondani (C)
6:Said Juma Makapu
7:Yusuf Mhilu
8:Papy Kabamba
9:Obrey Chirwa
10:Pius Buswita
11:Thabani Kamsoko

Kikosi cha Akiba
1:Ramadhan Kabwili
2:Abdallah Shaibu
3:Nadir Haroub
4:Juma Mahadhi
5:Raphael Daud
8:Ibrahim Ajibu
7:Geofrey Mwashiuya
12:50:00 PM

HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA AL MASRY (KOMBE LA SHIRIKISHO

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Kikosi cha kwanza cha Simba Sc kinachoanza dhidi ya Al Masry saa 20:30 usiku mchezo huu utakuwa live nijuzehabari ifikapo saa 20:30
1:Aishi Manula
2:Nicholaus Gyan
3:Asante Kwasi
4:Erasto Nyoni
5:Juuko Mrishid
6:Jonas Mkude
7:Shomary Kapombe
8:James Kotei
9:Emmanuel Okwi
10:John Bocco
11:Said Ndemla

Kikosi cha Akiba
1:Said Mohammed 'Nduda'
2:Mohammed Hussein JR
3:Paul Bukaba
4:Mwinyi Kazimoto
5:Mzamiru Yassin
6:Laudit Mavugo
7:Shiza Kichuya
10:01:00 AM

ROJO AJITIA KITANZI MANCHESTER UNITED HADI 2022

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Na Yego Sholla

Beki Marcos Rojo akisaini mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu leo kuendelea kuichezea Manchester United hadi mwaka 2022 na kuzima tetesi za Muargentina huyo aliyewasili Old Trafford mwaka 2014 kwa dau la Pauni Milioni 16 kutoka Sporting Lisbon kuhamia PSG kwa Pauni Milioni 30
10:00:00 AM

FATILIA MOJA KWA MOJA MECHI ZA SIMBA NA YANGA (MICHUANO YA KIMATAIFA) LIVE KWENYE BLOG YETU YA NIJUZEHABARI

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Habari mdau wa Nijuzehabari Blog hii ni habari njema kwako Mtanzania na mpenda soka, wakati timu za Simba na Yanga zikibakiza muda mchache kushuka dimbani kwa ajili ya michezo ya marudiano michuano ya kimataifa, nijuzehabari.co.tz itakuletea live michezo hiyo ikifika muda muafaka.

Leo Jumamosi ya March 17 itapigwa michezo mbalimbali ya kimataifa katika viwanja mbalimbali, ambapo timu za Tanzania Simba na Yanga zitashuka dimbani kuliwakilisha taifa katika michezo ya marudiano ya kimataifa barani Afrika.

Kuelekea mchezo wa mapema wa Township Rollers ya Botswana dhidi ya Young Africans ya hapa nchini nijuzehabari itakuletea kila kinachoendelea huko Botswana hadi dakika 90, mchezo huu utaanza majira ya saa 16:45 jioni kwa saa za hapa Tanzania.

Mchezo wa pili utakuwa kati ya Al Masry ya Misri dhidi ya Simba Sc ya hapa Tanzania pia mchezo huu utakuwa live nijuzehabaro.co.tz kuanzia majira ya saa 20:30 usiku kwa saa za hapa Tanzania.

Katika mchezo awali Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia magoli 2-0 ili kuweza kusonga mbele baada ya kupoteza nyumbani kwa jumla ya goli 2-1.

Simba wao wanaitaji ushindi wowote au sare yamagoli 3-3 ili kusonga mbele baada ya kutoa droo nyumbani ya magoli 2-2.

Ratiba kamili ya mechi za shirikisho leo Jumamosi ya March 17-2018 (Kwenye mabano ni matokeo ya awali)

APR (Rwanda) vs Djoliba (Mali) (0-1)

Hilal Obied (Sudan) vs Olympic (Burundi) (0-0)

Nkana (Zambia) vs CR Belouizdad (Algeria) (0-3)

Al Masry (Egypt) vs Simba (Tanzania) (2-2)

Club Africain (Tunisia) vs RS Berkane (Morocco) (1-3)

Nouadhibou (Mauritania) vs Raja Athletic Club (Morocco) (1-1)


Michuano hiyo itaendelea kesho Jumapili ya March 18-2018

Cape Town City (South Africa) vs Costa do Sol (Mozambique) (1-0)

Enyimba (Nigeria) vs Energie (Benin) (2-0)

Fosa Juniors (Madagascar) vs Port Louis (Mauritius) (2-0)

USM Alger (Algeria) vs AS Maniema (DR Congo) (2-2)

Deportivo Niefang (Equatorial Guinea) vs Motema Pembe (DR Congo) (1-1)

Akwa United (Nigeria) vs Al Ittihad (Libya) (0-1)

Ben Guerdane (Tunisia) vs CARA (Congo) (0-3)

Zamalek (Egypt) vs Wolaitta Dicha (Ethiopia) (1-2)


Ratiba kamili ya mechi za klabu bingwa Afrika leo Jumamosi ya March 17-2018 (Kwenye mabano ni matokeo ya awali)

KCCA (Uganda) vs Saint George (Ethiopia) (0-0)

Mbabane Swallows (Swaziland) vs Zanaco (Zambia) (2-1)

Williamsville (Cote d’Ivoire) vs Wydad (Morocco) (2-7)

CF Mounana (Gabon) vs Al Ahly (Egypt) (0-4)

MC Alger (Algeria) vs MFM (Nigeria) (1-2)

Generation Foot (Senegal) vs Horoya (Guinea) (1-2)

Township Rollers (Botswana) vs Young Africans (Tanzania) (2-1)

UD Songo (Mozambique) vs TP Mazembe (DR Congo) (0-4)

Bidvest (South Africa) vs Primeiro de Agosto (Angola) (0-1)


Michuano hiyo itaendelea kesho Jumapili ya March 2018

ES Setif (Algeria) vs Aduana (Ghana) (1-0)

Esperance (Tunisia) vs Gor Mahia (Kenya) (0-0)

Plateau United (Nigeria) vs Etoile du Sahel (Tunisia) (2-4)

El Hilal (Sudan) vs AS Togo (Togo) (0-2)

ASEC Mimosas (Cote d’Ivoire) vs Zesco (Zambia) (1-0)

AS Vita (DR Congo) vs Difaa El Jadidi (Morocco) (0-1)

Mamelodi Sundowns (South Africa) vs Rayon Sport (Rwanda) (0-0)
9:59:00 AM

MASWALI MUHIMU KUHUSU KESI YA WAMBURA NA TFF

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

HIVI karibuni kumetoka hukumu ya makamu wa Raisi wa Shirikisho la soka nchini (TFF, Michael Richard Wambura, ambaye alikuwa anakabiliwa na makosa matatu.

Kosa la kwanza ni kupokea fedha za shirikisho kwa malipo yasiyo halali. Kosa la pili ni kughushi barua ya kuelekeza malipo ya kampuni ya Jeck system Limited. Kosa la tatu ni kushusha hadhi ya shirikisho kwa alichokifanya kwenye makosa namba moja na mbili.

Kuna vitu ningependa tuviangalie kwa pamoja kuanzia jinsi kesi ilivyoanza mpaka hukumu ilivyotolewa. Michel Richard Wambura anahukumiwa kwa kosa la kwanza ambalo ni kupokea fedha za shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) yasiyo halali.

Ukiangalia katiba ya TFF iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2013 kwenye kanuni za maadili kifungu cha 73(1) kinamhukumu moja kwa moja Michael Richard Wambura.

Hapa kwa kanuni za kimaadili ya TFF zitakuwa zinamhukumu moja kwa moja Michael Richard Wambura. Swali la kujiuliza, Michael Richard Wambura amepatikana na hatia ya kupokea pesa za shirikisho kwa malipo yasiyo halali,ambalo kwa mujibu wa sheria za nchi ni kosa la jinai dhidi ya Jamhuri.

Sheria ya Makosa ya jinai Sura ya 16 ya sheria za Tanzania iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 inataja makosa ambayo ni dhidi ya Jamhuri pamoja na adhabu zake.

Sasa Jamhuri ni nini? Sheria hiyo katika sura yake ya pili inatoa maana ya Jamhuri kuwa “refers not only to all persons within Mainland Tanzania but also to the persons inhabiting or using any particular place, or any number of those persons, and also to such indeterminate persons as may happen to be affected by the conduct in respect to which such expression is used”

Kwa tafsiri ya lugha ya Kiswahili isiyo rasmi Jinai ni kosa au makosa yanayofanywa na mtu/watu/taasisi kupitia watendaji wake, kinyume cha sheria au taratibu zilizoainisha makosa mabalimbali. Kwa mfano makosa yote yaliyoainishwa katika sheria ya kanuni za adhabu Sura ya 16.

Sasa katika kosa la kwanza la Michael Richard Wambura, ni kupokea fedha za shirikisho ya malipo yasiyo halali, hii moja kwa moja ni kosa la jinai.

Kosa ambalo linatambulika na sheria za nchi kama ilivyoainishwa katika sheria ya sura ya 16. Katika hilo tumwachie Mwendesha Mashataka mkuu wa Serikali alitafutie ufumbuzi dhidi ya Michael Wambura kwa sababu mambo ya soka hayapelekwi mahakamni.

Kosa la pili alilopatikana nalo Michael Richard Wambura ni la kughushi barua ya kuelekeza malipo ya kampuni la Jeck System Limited yafanyike kupitia yeye.

Hatua hiyo ni kinyume na kanuni za maadili ya TFF, kifungu cha 73(7) cha kanuni ya maadili ya mwaka 2013. Kosa hili kwa mujibu kwa sheria za nchi ni la jinai.

Kama inavyojulikana kwa sheria ya Jamhuri kosa la jinai linatambulika kama nilivyoelezea huko juu. Hili nalo liko mikononi mwa mwendesha mashtaka Mkuu wa serikali kulifanyia kazi. Hapa Shirikisho la soka TFF wamefungua njia.

Kosa la tatu na la mwisho kwa mujibu wa Kamati ya maadili ya TFF linasema Michael Richard Wambura ni kushusha hadhi ya shirikisho kwa alichokifanya kwenye makosa namba 1 na 2. Hii ni kinyume na kifungu cha 50(1) cha makosa ya jinai.

Katika sheria za nchi kosa hili linachukuliwa kama kosa la ‘Defamation’ ambalo kwa tafsiri ambayo isiyo rasmi linajulikana kama “Kudhalilisha”.

Sheria mpya ya huduma za habari ya mwaka 2016 (The Media services Act, 2016) ambayo imefuta sheria ya Magazeti (The Newspapers Act, No.3 of 1976) imeainisha kosa hili katika sura ya tano.

Kwa mujibu wa Ibara ya 35 katika kifungu kidogo cha 1 cha sheria ya Huduma za habari imefafanua kuwa “Defamation” ni jambo lolote ambalo likichapishwa na kusambazwa linaweza kuharibu hadhi ya mtu, au utu wake au kuibua chuki dhidi yake au kuharibu kazi au fani ya mtu huyo. Ni jambo la kudhalilisha.”

Nanukuu: Section 35(1) “any matter which, if published, is likely to injure the reputation of any person by exposing him to hatred, contempt or ridicule, or likely to damage any person in his profession or trade by an injury to his reputation, is defamatory matter”.

Hivyo basi kudhalilishwa ni hali inayojitokeza kwa mtu yoyote pale ambapo jambo hilo limechapwa na kusambazwa dhidi yake na kusababisha kuharibu hadhi ya mtu huyo, utu wake au kuibua chuki dhidi yake au hata kuharibu kazi au fani ya mtu huyo.

Kwa mujibu wa kifungu tajwa hapo juu mtu yeyote anayelalamika kuwa amedhalilishwa ni lazima ithibitike/athibitishe mbele ya mahakama.

Kimsingi makosa mawili ya mwanzo ya Michael Richard Wambura yamedhalilisha shirikisho la mpira Tanzania ( TFF) pamoja na wapenda mpira.

Kwa upande wa Michel Richard Wambura anatakiwa atujibu maswali yafuatayo; Ni kweli aliomba mkopo wa kifedha kutoka kwa kampuni la Jerkers System Limited bila idhini ya kamati ya utendaji?

Na kama jibu ni ndiyo kampuni ya Jerkers System Limited linajihusisha na utoaji wa mkopo? Sheria za mikopo zinaruhusu taasisi ipi itoe mikopo?

Kwanini malipo yafanyike kipindi ambacho yeye alikuwa madarakani na kipindi ambacho kinachosemekana marafiki zake (Rais Jamal Malinzi) walipokuwa madarakani? Kwanini kipindi cha Raisi Leodegar Chilla Tenga malipo hayakufanyika?

Mathalani ile barua JKC/SONT/TFF/2014 ya tarehe 13/01/2014 inayoonesha Michael Wambura ameidhinishwa na kampuni ya Jeck System Limited, kwanini inakanwa na mke wa marehemu (kwa sasa ndiye msimamizi mkuu wa mirathi) ambaye alikuwa mmiliki wa kampuni hiyo?

Wakati tukisubiri majibu ya Wambura tunatakiwa pia tupate majibu ya TFF kwenye maswali yafuatayo; Mosi, kwa mujibu wa kanuni za maadili namba 48 ya TFF ya mwaka 2013 inaainisha kuwa barua ya wito inatakiwa ipelekwe siku tatu kabla ya siku ya kusikilizwa kwa kesi. Je ni kweli walipeleka barua siku moja kabla ya kesi kusikilizwa, kama ni kweli hawaoni kuwa walifanya makosa hivyo kuvunja kanuni za maadili ya TFF?

Kwa mujibu wa kanuni ya 58 ya maadili ya TFF ya mwaka 2013 inaainisha kuwa mtuhumiwa anapofika mbele ya kamati anatakiwa apewe siku za kukusanya ushahidi na mashahidi wa kesi husika, lakini kwa mujibu wa mwanasheria wa Michael Richard Wambura hii kanuni haikufuatwa, tunatakiwa tujue ni kwanini haikufutwa?

Michael Richard Wambura kahukumiwa bila kujitetea mbele ya kamati, kwanini kamati haikumpa nafasi ya kujitetea? Kuna ufafanuzi wa matumizi ya bilioni 3 ndani ya miezi saba, kuna haja ya TFF kutoka nje na kuonesha matumizi ya pesa hizo kama ni kweli.

Kaimu katibu mkuu wa TFF ni kiongozi wa chama cha makocha Tanzania (TAFCA). Kwa mujibu wa kanuni anaingia moja kwa moja kama mjumbe wa Kamati Kuu ya TFF, ambapo ukiwa mjumbe wa kamati kuu hutakiwi kuwa mwajiriwa wa shirikisho la soka, hivyo kaimu katibu mkuu wa TFF anakosa sifa za kuajiriwa. Vilevile TFF inatakiwa ije mbele yetu na kututhibitishia kuwa Kaimu Katibu mkuu yupo kama mtu anayejitolea kama ilivyo kwa Afisa Habari?
9:55:00 AM

NIJUZEHABARI INAZITAKIA KILA LA HERI WAWAKILISHI WA TANZANIA SIMBA SC NA YANGA SC

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Na Yego Sholla

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Afrika, Simba na Yanga leo wapo ugenini kwa michezo ya marudiano ya hatua ya 32 Bora.

Yanga watakuwa wageni wa Township Rollers Uwanja wa Taifa mjini Gaborone, Botswana kuanzia Saa 10:45 jioni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa na Simba watakuwa wageni wa Al Masry Uwanja wa Port Said nchini Misri kuanzia Saa 2:30 usiku.

Yanga wanahitaji lazima ushindi wa mabao 2-0 ili kwenda hatua ya makundi, baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumanne ya wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba SC wanataka ushindi wowote, hata wa 1-0 ili kusonga mbele katika hatua ya mwisho ya mchujo baada ya sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.

Yanga ikiitoa Rollers itakwenda hatua ta makundi ya Ligi ya Mabingwa, ambayo kihistoria itakuwa mara yake ya pili baada ya mwaka 1998, lakini tolewa itaingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Simba SC ikishinda leo itacheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho, lakini ikitolewa itarejea nyumbani moja kwa moja.

Kila la heri wawakilishi wetu. Mungu zibariki Simba na Yanga. Mungu ibariki Tanzania. Amin.
9:55:00 AM

HUNA SABABU YA KUAIBIKA TENA JIPATIE DAWA ASILI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO SASA LINATIBIKA.

Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka na dalili nyingine kama hizi👇👇

1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZO HAPO JUU BASI UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Dk Kihembe amekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za OZYMIX POWER- ni dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.

PIA KUNA DAWA YA KUNENEPESHA NA KUREFUSHA MAUMBILE YA KIKE NA DAWA ZA KIKE ZA KUTENGENEZA SHEPU KAMA HIZI 👇👇

1: Kusimamisha maziwa yaliyolala
2: Kuongeza makalio
3: Kuondoa michirizi
4: Kumrudisha mwanaume aliyekuacha au Asiyekupa hela.

TUPO DAR ES SALAAM- KAWE. HUDUMA HII UNALETEWA POPOTE ULIPO KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM

WASILIANA NASI KWA SIMU: TIGO NO: 0716096205/ VODA NO: 0756726865 AU FIKA KATIKA OFSI ZETU ZILIZOKO KAWE


KWA MIKOANI TUNAKUTUMA KWA NJIA YA MABASI-DK KIHEMBE
8:40:00 AM

RATIBA YA SOKA LEO JUMAMOSI MARCHI 17

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Africa: CAF Champions League
16:00 KCCA vs St George Agg (0-0)
16:00 UD Songo vs TP Mazembe Agg(0-4)
16:00 Mbabane Swallows vs Zanaco Agg(2-1)
16:45 Township Rollers vs Yanga Sc Agg(2-1)
17:30 Mounana vs Al Ahly Agg(0-4)
18:00 Bidvest Wits vs 1° de Agosto Agg(0-1)
19:00 WAC vs Wydad Casablanca Agg (2-7)
20:30 Génération Foot vs Horoya Agg(1-2)
22:45 MC Alger vs Mountain of Fire Agg(1-2)

Africa:- CAF Confederation Cup
16:00 Nkana vs Belouizdad Agg(0-3)
16:30 APR vs Djoliba Agg(0-1)
17:00 Club Africain vs RSB Berkane Agg(1-3)
18:30 FCNDB vs Raja Casablanca Agg(1-1)
20:00 Hilal Obayed vs Olympic Star Agg (0-0)
20:30 Al Masry vs Simba SC Agg(2-2)

England:- Premier League
18:00 Bournemouth vs West Bromwich
18:00 Huddersfield vs Crystal Palace
18:00 Stoke City vs Everton
20:30 Liverpool vs Watford

England:- FACup
15:15 Swansea City vs Tottenham Hotspur
22:45 Manchester United vs Brighton

Hispania:- LaLiga
15:00 Deportivo La Coruña vs Las Palmas
18:15 Valencia vs Alavés
20:30 Real Sociedad vs Getafe
22:45 Real Betis vs Espanyol

Germany:- Bundesliga
17:30 Augsburg vs Werder Bremen
17:30 Frankfurt vs Mainz 05
17:30 Hamburg vs Hertha BSC
17:30 Borussia M'gladbach vs Hoffenheim
20:30 Wolfsburg vs Schalke 04

Italia:- Serie A
20:00 Udinese vs Sassuolo
22:45 SPAL vs Juventus

Ufaransa:- Ligue1
19:00 Bordeaux vs Rennes
22:00 Amiens vs Troyes
22:00 Angers vs Caen
22:00 Montpellier vs Dijon
22:00 Toulouse vs Strasbourg


12:59:00 AM

SIMBA YAKWEPA HUJUMA ZA WAARABU

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Mabosi wa Simba wameshtukia jambo na kuamua kufanya maamuzi magumu ya kuwabadilishia wachezaji wake ratiba ya chakula cha mchana leo Ijumaa mjini hapa.

Mabosi hao chini ya usimamizi wa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Tryagain' wamesitisha mchakato wa nyota wake kupata chakula cha mchana hapa kwenye hoteli ya Nora and Style waliyoshukia kwa hofu ya kufanyiwa hujuma na wenyeji wao Al Masry.

Mabosi hao wameagiza chakula kutoka hoteli nyingine kwa ajili ya wachezaji wake ili kukwepa fitna za wenyeji wao hao ambao wanasifika kwa kutafuta ushindi kwa njia za mkato.

Simba itacheza mchezo wake wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya hapa Port Said, Misri kesho Jumamosi usiku hivyo mabosi hao wameanza kupata hofu ya hujuma na kuamua kufanya mambo tofauti. Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam.

Mbali na hilo, wamepiga marufuku mtu yeyote asiyekuwa Mtanzania kuingia kwenye vyumba vya wachezaji na pia kuzungumza chochote na wenyeji wa hapa.

Credit: Mwanaspoti
12:54:00 AM

HANS POPPE ATUA MISRI KUKIONGEZEA NGUVU KIKOSI CHAKE

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amtua jijini Port Said kuungana na kikosi cha Simba jana Ijumaa ya March 16-2018.

Kikosi cha Simba Sc kinashuka dimbani leo saa 20:30 usiku huko Misri kuikabili Al Masry kwenye mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika

Hans Poppe amewasili Port Said mchana wa jana na kuungana na viongozi wengine wa Simba wakiwemo Kaimu Rais, Salim Try Again na Kaimu Makamu wake, Iddi Kajuna.

Pia wako wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Musley Al Rawah pamoja na Said Tuli

Katika mchezo huo Simba inahitaji ushindi wowote au sare ya magoli 3-3 ili kusonga mbele katika hatua ya makundi.
12:38:00 AM

BAADA YA KUFUNGIWA MAISHA MICHAEL WAMBURA AKATA RUFAA

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Wakili wa makamu wa Rais wa Shirikisho la soka nchini Emmanuel Muga, amethibitisha kukamilisha taratibu zote za kumkatia rufaa mteja wake Michael Richard Wambura ili shauri lake liweze kusikilizwa tena.

Muga amesema katika rufaa hiyo wamewasilisha mambo matano ambayo wameomba yasikilizwe kwa hati ya dharula kwani mteja wake (Michael Richard Wambura) ni mtu mwenye majukumu mengi ya kitaifa na kimataifa.

“Rufaa hiyo tumeomba isikilizwe kwa hati ya dharula kwa sababu Wambura ni kamishna wa mechi wa shirikisho la soka Afrika na mwezi ujao ameteuliwa kuwa kamishna kwenye mechi ya Rwanda na Kenya, lakini pia ni kiongozi wa mkoa na kitaifa pia,” Muga ameeleza.

Muga ambaye aliwahi kuwa mwanasheria wa TFF siku za nyuma amesema miongoni mwa mambo waliyoyakatia rufaa ni kuhoji uhalali wa kamati iliyomtia hatiani mteja wake ambapo kikanuni haina mamlaka ya kufanya maamuzi hayo.

“Moja wapo ya sababu ya rufaa ni kuwa kamati haikuwa na mamlaka ya kufanya walichokifanya, sababu nyingine kamati haikufuata sheria na katiba ya TFF wakati inafanya maamuzi, pia kamati haikumpa Wambura nafasi ya kusikilizwa na pia kamati hakupokea ushahidi wowote walijiamulia tu,” Muga amesema.

MAKOSA YAKE
Ikumbukwe kuwa mchana wa Machi 15, 2018 Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), ilimfungia maisha kutojihusisha na shughuli za soka Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura.

Inadaiwa kuwa Wambura amefungiwa kutokana na kupokea fedha zisizo halali kiasi cha Shilingi milioni 84, pamoja kughushi nyaraka za malipo, na kula njama kulipwa fedha na waliokua viongozi wa TFF Jamal Malinzi na Selestin Mwesigwa.
12:17:00 AM

THABANI KAMUSOKO AIPANIA TOWNSHIP ROLLERS

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Kiungo wa Yanga Thaban Kamusoko amesema kikosi cha timu hiyo kipo katika hali nzuri, tayari kupindua matokeo na kuichapa Township Rollers katika mchezo wa leo utakaofanyika huko Botswana.

Kamusoko ametoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya wanahabari, katika mkutano (Press Conference) uliofanyika jana nchini humo.

"Township Rollers ni timu nzuri tunaiheshimu na tumeona mpira wake kikubwa naamini tumejipanga kuibuka na ushindi kwa kuwa mwalimu amefanyia kazi makosa yote ya mchezo uliopita," aliongeza Kamusoko.

Katika mchezo wa awali uliofanyika jijini Dar es salaam March 07 mwaka huu, Yanga ilifungwa magoli 2-1 kutoka na matokeo hayo Yanga inalazimika kutafuta ushindi  wa goli 2-0.

Habari njema ni kuwa pamoja na kuwa live Azam Tv, mchezo huo pia utakuwa live hapa hapa nijuzehabari tukikuwekea updates za dakika 90 zote kuanzia saa 16:45 jioni.
12:02:00 AM

ALICHOKISEMA NIYONZIMA BAADA YA KUREJEA RASMI

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOK, TWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA

Hii inaweza kuwa ni habari njema kwa mashabiki wa Simba baada ya nyota wao, Haruna Niyonzima aliyekuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu wa kulia, sasa karejea tena uwanjani.

Akizungumza jana, Niyonzima amethibitisha yupo fiti na ataanza mazoezi na wenzake mara watakaporejea kutoka Misri watakakokocheza keshokutwa Jumamosi mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry.

“Sasa niko fiti, naweza kurudi uwanjani, nadhani wenzangu watakaporejea kutoka Misri tu nitajiunga nao mazoezini,” alisema Niyonzima jana kwa furaha.

Kiungo huyo fundi ambaye alikubalika kwa mashabiki wa Simba alipojiunga na timu hiyo akitokea Yanga mwanzoni mwa msimu huu, alisema anarejea upya uwanjani na anaamini mambo yatakuwa mazuri tena kwake.

“Matatizo ni sehemu ya maisha, lakini nashukuru Mwenyezi Mungu amenisimamia na sasa nimepona na bila shaka nitarudi uwanjani mapema wenzangu watakaporejea nchini,” alisema.

“Naendelea na mazoezi binafsi, niko ‘bomba sana’ akimaanisha yuko fiti na bahati iliyoje sikufanyiwa upasuaji kama ilivyotarajiwa nilipokwenda India.

“Kule nilipewa matibabu mbadala na ninaendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu tiba imenisaidia na ninaendelea vizuri,” alisema kiungo huyo Mnyarwanda.

Akizungumzia matibabu yake India, Niyonzima alisema yalienda vizuri na alianza kupatiwa tiba mbadala iliyofanyika kwa siku 10 kisha madaktari wakabaini hana haja ya kufanyiwa tena upasuaji.

“Hilo lilikuwa jambo la kumshukuru Mungu pia, maana upasuaji nao ni kitu kingine, bahati nzuri tiba niliyopewa nje ya upasuaji imenisaidia na sasa niko tayari kurudi uwanjani,” alisema.

Kiungo huyo amekuwa na msimu mbaya tangu amejiunga na Simba akiwa hajafunga wala kusaidia bao lolote katika mechi chache alizocheza kabla ya kuumia.